RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MH LAZARO NAYANDU AWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA ALBAM MPYA YA CHRISTINA SHUSHO-DAR ES SALAAM

Mwandishi: Rumafrica
Kazi ya Bwana ilifanyika katika viwanja vya kanisa la Pentekoste Tabata Kisiwa jijini Dar es Salaam Tanzania na kuhudhuriwa na watu wengi sana. Tamasha la uzinduzi wa albamu ya mtumishi wa Mungu Christina Shusho lilianza saa nane mchana siku ya Jumapili 02/03/2015. Watu walikaa pamoja wakifurahia uwepo wa Mungu uliotanda eneo hilo. Mungu alionekana akiwa mlinzi kwa wana wa Mungu waliofika siku hiyo.

Wapili kutoka kushoto ni Christina Shusho akifuatiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyarandu wakiserebuka

Mgeni  Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lozaro Nyarandu aliweza kuserebuka na kuacha watu wakiwa wameachama mdomo wazi wakishangaa kuona hata viongozi wa serikali wanaweza kuserebuka na kumtukuza Mungu. Hii inatokana na vile nyimbo za mwadada huyu kuwa na kibali kwa kila mtu na upako alionao. Mh. Nyarandu ni waziri ambaye amekuwa mstari wa mbele sana katika kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele, amekuwa mwepesi pale anapoombwa kushiriki katika sherehe na matamasha mbalimbali ya dini. Uwepo wa Mh. Nyarandu uliwafanya watu kubarikiwa sana kutokana na unyenyekevu wake na upole mbele za watu. Mh. Nyarandu hakijizuia na aliweza kutoa dola zake mfukoni na kumponeza Christina Shusho wakati akiimba, hii inatokana na kuguswa na uimbaji wake.
 Wapili kutoka kushoto ni Christina Shusho akifuatiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyarandu wakiserebuka
Kitu ambacho nilijifunza katika tamasha hili ni ule upendo aliokuwa nao Christina Shusho kwa watu na pia kazi zake kuwa nzuri na zenye ujumbe ambao unagusa maisha ya watu. Christina Shusho ni mwimbaji anamtumainia sana na pia ni mtu anayefanya kazi kwa bidii kuhakikisha kazi ya Mungu inakwenda mbele ikiwa katika viwango vya kimataifa machoni pa watu na mbele za Mungu. Mungu amekuwa akimbariki sana na kuweka upako katika albamu zake, na ndio maana ukisikiliza nyimbo zake hutamani kutoa CD au DVD ndani ya deki yako.
 Tamasha hili lilitakiwa lifanyike ndani ya kanisa lakini kutokana na watu wengi ikabidi lifanyike nje ya kanisa. Tuone baadhi ya picha.


 Christina Shusho (kushoto) Mh. Lazaro Nyarandu (wa pili kustoka Kushoto)




 Christina Shusho (kushoto) na mdau wake


 Emmanuel Mabisa (kulia) na Christina Shusho (kushoto)
 Emmanuel Mabisa (kulia) na Christina Shusho (kushoto)

Picha zimepigwa na Emmanuel Mabisa

Comments