RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

GWT SUNDAY CELEBRATION SEASON 6 NDANI YA UKUMBI WA VICTORIA -DAR ES SALAAM


Erick Shigongo akifundisha

Mungu akisema NDIYO, hakuna wa kupinga, hii imetokea kwa vijana machachari wa Yesu, nao ni Glorious Worship Team ambao hawachoki kumtumikia Mungu kwa nyia ya aina yake. Baada ya kutaabika kwa muda mrefu sana na kuwa kimia, Mungu aliweza kufungua milango kwa vijana hawa na kupata mtu wa kuwasukuma mbele ambaye si mwingine ni Mkurugenzi wa Global Publishers Tanzania, Erick Shigongo. Amekuwa msaada mkubwa sana kwa vijana hawa, na pia amekuwa akifundisha masomo ya kujikwamua na UMASKINI katika kusanyiko hili la SUNDAY CELEBRATION.

Imma Bezi

Jumapili ya 26/04/2015 waliweza kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji, watu waliweza kufika na kumtukuza Mungu. Hakika Mungu ni mwema kwa vijana hawa. Wanahitaji sana maombi yenu ili huduma hii izidi kusonga mbele kwa kazi ya Mungu. Pia wanahitajisapoti yako ya kimawazo na hata financially kama unabarikiwa na huduma yao.

GWT wanafanya event zao bure kabisa kila Jumapili katika ukumbi huu wa Victoria. Wanaamini kubarikiwa kwako ni utukufu kwa Mungu. Kufika kwako ndiko kunawafanya wazidi kufanya vitu vikubwa vyenye kumtukuza Mungu wetu. Unaombwa sana kuwajulisha na wengine ili waweze kufika na kumtukuza Mungu baada ya ibada kumalizika. Mara nyingi event huanza saa 8:00 mchana na kuendelea bila ya kiingilio na unapata somo kutoka kwa Eric Shigongo jinsi ya kujikwamua katika wingu la UMASKINI.


Mwanafunzi na kitabu

Danny Mbepela ndani Jordan TEAM

wanafunzi wakimsikiliza Ticha kwa Makini


Ticha Shigongo akitoa Nondo Darasani





Danny Kibambe katika Worship na GWT

Emma Mabisa MD wa GWT katika Praise



Davina



Ester

Comments