RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JESHI LA NIGERIA LAWAOKOA MATEKA 293 WA BOKO HARAM



Jeshi la Nigeria likishambulia ngome za Boko Haram katika msitu wa Sambisa.
Wanajeshi wa Nigeria wakiimaklisha ulinzi dhidi ya Boko Haram nchini humo.

Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa wasichana 293 kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema kuwa, wasichana hao waliokolewa siyo wale waliotekwa na kundi hilo mwaka jana katika eneo la Chibok.

Akizungumza na vyombo vya habari, msemaji wa Jeshi limeiambia limeongea na vyombo vya habari kwamba, wanawake na wanawake na wasichana hao walikutwa katika kambi nne tofauti Boko Haram ambapo silaha pia zimekamatwa, ameongeza kuwa, Jeshi liliwapata mateka hao baada ya kuzivamia na kuzishambulia kambi kisha kufanikiwa kuwaokoa.

"Ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu." Alisema kiongozi huyo.

Kwa sasa Jeshi limezuiwa kutoa kuweka wazi majina ya mateka hao waliookolewa kusisitiza kuwa wasichana hao siyo wale wanafunzi waliotekwa katika mji wa Chibok mwaka jana.

Msemaji wa Jeshi la Nigeria alisisitiza kwa kusema, "Tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote."
NA BBC

Comments