RUMAFRICA Jumapili ya 05/04/2015 ilibahatika kuhudhuria ibada ya pili katika kanisa la EFATHA Mwenge jijini Dar es Salaam. Ibada ilianza saa 4:00 asubuhi na kumalizika saa 7:00 mchana. Somo lililofundishwa ma Mchungaji ambaye Rumafrica haikubahatika kupata jina lake, somo lilikuwa ni mwendelezo wa somo la Jumapili mbili zilizopita nalo lilikuwa:
Nabii Josephate Mwingira na mke wake mama Eliyapunda Mwingira katika kongamano la Viongozi.
UTAKATIFU
Utakatifu ni kutii maagizo ya Mungu. Huu ni mwaka Mtakatifu tunatakiwa kutembea katika Utakatifu wake. Mungu wetu ni Mtakatifu hataki mtu kuwa mchafu au mtu ambaye ni vuguvugu, kwani ukiwa vuguvugu atakutapika tu.
Usipokubali kuwa Mtakatifu, Yesu anasema, atakutapika. Tunachotakiwa kumwambia Yesu Kristo ni kwamba atupe hatua nyingine ili tuwe Watakatifu na tutembee naye. Kila iitwapo leo tamani Bwana akupe hatua nyingine ili tuwe watakatifu, na usisahau kutembea naye kila mahali unapokwenda au kuwepo.
Utakatifu ni maamuzi ya mtu binafsi. UTAKATIFU ni kutii maagizo ya Mungu. Mungu anatumia watu kuleta maagizo yake, pale unapoambiwa na viongozi wako kanisani kwako unatakiwa kutii kwasababu wametumwa na Mungu kwa kazi YAKE.
Baadhi ya maagizo ya Mungu yaliyo ndani ya kanisa la EFATHA ni kama yafuatayo

- Kumbuka siku ya Bwana na kufika katika nyumba ya ibada na usisubiri mtu akukumbushe siku ya ibada. Unatakiwa kuwahi ibadani na huo ndio utii
- Kutoa fungu la kumi kwaajili ya Injili kusonga mbele. Ni maamuzi yako ya kutoa kwa Mungu ili akubariki, usiongozwe na mtu akulazimishe kutoa
- Kukaa darasani kwako wewe ambaye umeokoka kwa mara ya kwanza. Unapokaa darasani unapata uwezo wa kufukuza mapepo, na unajifunze Neno la Mungu na baadae unafanyika msaada kwa wengine. Hudhuria vipindi tangia umejiandikisha kuanza darasa lako la kukulia wokovu. Unatakiwa kutii maagizo. Tamani kusoma Neno la Mungu na baadae hubiri Neno la Mungu.
- Fungua akaunti yako katika Benk ya EFATHA ili iweze kuongezeka na kuwa mfano kwa mataifa.
- Kata BIMA katika Insurance Center yetu ya EFATHA. Tamani sana kuunga mkono huduma zinazoanzishwa katika kanisa lako ili liweze kukua na kuweza kusaidia na wengine wenye uhitaji.
- Hudhuria kambi zinazoatangazwa hapa kanisani kama vile kambi ya NDOA. Kuna baadhi ya wanandoa hawakuweza kwenda kwenye kambi ya NDOA na hivyo hawakutii maagizo ya Mungu. Umeshindwa kutenga muda wa kuhudhuria kambi hii na sasa unalalamika kuwa ndoa yako inayumbayumba.
- Kuhudhuria kusanyiko litakalofanyika mwezi wa kumi mwaka huu. Unatakiwa kujiandaa mapema ili siku hiyo kusiwe na kipingamizi.
- Kuwaleta watu kanisa ili waokoke. Katika kanisa letu tumesema kila muumini alete mtu kanisani aokoke. Watu wengine wamewaleta watu kanisani lakini wameshindwa kwalea na kusababisha warudi katika imani yao ya awali. Unapomleta mtu kanisani jaribu kumkazania aimarike kiroho na baadae ajitegemee.
- Mahali popote palipo Patakatifu Mungu yupo hapo. Soma Daniel 3:19-27. Pamoja na vikwazo unavyopitia lakini ukiwa Mtakatifu utashinda tu. Ukishaamua kuishi maisha ya utakatifu unaweza kuwakimbiza wale wote wanaokujia wewe kukukatisha tamaa kumtumikia Mungu. Wakikuona wanaona uko serious na kazi ya Mungu na huwaungi mkono kwa mambo yao ya kipuuzi, kwasababu hupendi kuondoa utakatifu wako
Wewe uliyeamua kutembea na Mungu katika Utakatifu, ujue kuna vishawishi na hivyo unatakiwa kuvishinda kwa kuwa na msimamo wako. Ukiwa na msimamo unapata usaidizi wa Mungu.
Jambo ukiamua mwenyewe ni rahisi kulitekeleza. Yule Mtakatifu wa Watakatifu ataleta usaidizi. Kuna wakati Mungu anataka ujidhihirishe kuwa wewe ni mfuasi wake. Ukiamua kuwa Mtakatifu, shida yako au mshale juu ya maisha yako utaondoka kwasababu una nguvu ya Mungu
Comments