RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA EFTHA MWENGE: KUWAKUMBUKA WALIOKUSAIDIA NA KUSAIDIANA

Rumafrica kwa mara ya kwanza tangia mwaka uanze wa 2015 haikuweza kubahatika kumuona Nabii na Mtume Josephate Mwingira akihubiri katika ibada zote za Mwaka 2015. Siku ya Jumapili ya 12/04/2015 Nabii na Mtume Josephate Mwingira aliweza kusimama madhabahuni na kushangiliwa sana na waumini wake kutoka na ku-miss kwa muda mrefu sana.

Picha ya Nabii na Mtume Josephate Mwingira (kushoto) na mke wake Eliyapunda wakiwa katika ibada za mikoani.

Nabii na Mtume Josephate Mwingira alikuwa ahubiri kutokana na majuku aliyokuwa nayo ya kufanya mikutano mikoani, na hii ilimsababishia kutoweza kupata muda wa kuhubiri katika kanisa lake baba la EFATHA (Funguka) lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam katika kituo cha mabasi ya Tegeta.

Nabii na Mtume Josephate Mwingira aliweza kufundisha somo ambalo lilikuwa ni mwendelezo wa somo alilowahi kuhubiri kwa mara ya mwisho kanisani kwake kabla ya kuanza mikutano ya mikoani. Somo lilihusu sana:


 KUWAKUMBUKA WALIOKUSAIDIA NA KUSAIDIANA


Tusome  Yohana 1:6-21.

SURA YA KWANZA ULIYOSOMA KATIKA YOHANA 1:6-1
Kitu kilichosababisha watu wamfuate Yesu ni Ishara na miujiza. Mahali popote Yesu alipo kuna msaada na usaidizi. Yesu ni kimbilio kwasababu anatosheleza hitaji lako kwa matendo.
 
SURA YA YA PILI ULIYOSOMA YOHANA YOHANA 1:6-21
Katika sura hii tunajifunza USAIDIZI kama vile Philipo na Andrea. Yesu alihitaji sana watu wa kumsaidia kazi. Palipo Yesu pana usaidizi kwaajili ya kufanya mambo ya kawaida. Kiongozi yoyote lazima awe msaidizi, kiongozi lazima atoe msaada kwa watu wengine. Mungu wetu hatumii silaha au bunduki bali hutumia maneno. Serikali ambayo inatumia bunduki mara nyingi haidumu.

Watu wanatakiwa kuwajibika kwenye nafasi zao. Ukiwajibika katika nafasi yako, ndipo Mungu anaingilia na kufanya maajabu yake. Usitegemee kupata kitu kutoka kwa Mungu wakati hufanyi kazi katika nafasi yako. Unaweza kuwa mtu wa maombi sana lakini hufanyi bidii katika nafasi yako, basi hautapata chochote. Unapofanya majukumu yako muujiza na nafasi ya Mungu unajitokeza.

SURA YA TATU ULIYOSOMA KATIKA KITABU CHA YOHANA 1:6-21
Katika sura hii tunajifunza "TUSISAHAU KILICHOTUSAIDIA HADI HAPA TULIPOFIKA". Usisahau wazazi wako, walimu wako, kwani wamekufikisha hapo. Hakikisha unamkumbuka aliyekufundisha kujua A, E, I, O, U, muombee kama bado anaishi. Walimu wanaishi maisha magumu sana na inafika wakati watu wanawatuma askari kuwapiga walimu wanapodai haki zao.

Yesu Kristo anasema "angalieni kisipotee kitu chochote" Tunaamini ipo siku Mungu ataikomesha hali hii ya unyanyasaji na kwatesa watu waliowasaidia mlipokuwa na uhitaji. Tuache pia tabia ya kuwatesa madaktari, na tukifanya hivyo kwa kuwatesa ipo siku Mungu atatupa kipigo.

Kila  hatua unayopitia ujitahidi kuitunza. Usipoteze chochote ambacho ambacho kilikutoa mahali fulani kwenda mahali pengine. Hata kama ndugu yako alikuleta mjini na baadae akakufukuza, ukifanikiwa kimaisha usimsahau, matafute na umpe zawadi.

Mungu wet9u anapenda sana kukuona unakumbuka ulikotokea. Unatakiwa kumsaidia aliyemdogo na aliyemkubwa. Ukisoma katika Zab 128, mizeituni kazi yake ni kutoa matunda ya upako. Tamani kutunza patakatifu pa Mungu wetu ili paweze kutoa matunda ya upako, na ukifanya hivyo utakuwa bora. Tamani kuwa na upendo kwa watu wote hasa waliokusaidia na wale ambao hawakukusaidia, na Mungu atakubariki sana.

Unapofanya majuku yako unaruhusu Yesu kukufikisha unakotaka kwenda, unapewa masaidizi wa kukusaidia. Unaweza kufanya jambo kwa muda mrefu bila ya mafanikio, lakini kwa kupitia wasaidizi wa Mungu utashangaa amekuwezesha kufanya kwa muda mfupi.

Unapofanya vizuri, Mungu anakupa msaidizi wa kukupeleka. Mungu akusaidie akufikishe unakokwenda. Amen

Mwandishi
Rumafrica
+255 715 851 523


Comments