RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MACHUFUKO TANZANIA, KENYA, NIGERIA NA BAADHI YA SEHEMU ZA AFRICA YASABABISHA SOLLY KUIMBA KWA MUDA MREFU TAMASHA LA PASAKA 2015 TANZANIA


Kuna ukweli kuwa kuna mambo mengi yanatusonga lakini haina maana kuwa suluhisho la matatizo hayo ni kuuwa watu wasio na hatia, hatuwezi kuwauwa watu weusi au kuwaua waafrika wasio na hatia. Kuna kila dalili kuwa wapo watu wanaotaka kuaminisha wengine kuwa Afrika ni bara dhaifu, halina utulivu pia hatuna muda wa kujadili mambo yetu,hatuwezi kujitawala, hatuwezi kuamua mambo yetu kwa hali ya amani na utulivu.
Ni vyema kutambua kuwa afrika ilikuwapo kabla ya afrika kusini, na watu weusi tulikuwapo kabla ya afrika kusini.
Nimerejea hivi majuzi kutoka nchini Tanzania ambapo nilihudhuria tamasha kubwa kabisa la kiinjili mnamo april 5, watu walifurika wengi sana kuja kuniona pia nilipata nafasi ya kupanda jukwaani japo kwa muda mchache na hii ni kwa sababu kulikuwa na tishio la mashambulizi ya kigaidi la alsha baab.

Wenyeji wangu walinitaka nisitumie muda mrefu jukwaani kwa sababu za kiusalama.lakini pia Nigeria kuna mashambulizi ya boko haram na serikali yao haijui lini itawaachia wasichana waliotekwa.
Hivi vyote ni viashiria vya kuonesha kuwa bara la afrika limevamiwa na watu tunaishi hatuna amani basi tuuungane kwa pamoja na tumshinde shetani na hila zake,wote kwa pamoja tukemee pepo hili la mauaji ya xenophobia, alshaabab, bokoharam na kwa kuomba kwa pamoja .
tushikane mikono na kila mmoja amshike jirani yake na tuombe kwa dhati kabisa.


Comments