RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PICHA ZA UANDAAJI WA DVD YA MARTHA MWAIPAJA NA MDOGO WAKE BEATRICE MWAIPAJA NDANI YA KIGAMBONI -DAR

Ndugu hawa wameamua sasa kuja katika ujio mpya wa kushirikiana katika kutoa kitu kizuri kwaajili ya utukufu wa Mungu. Kwa kabila ni Wanyakyusa wa Mbeya ambao wamekuwa mstari wa mbele sana kumtumikia Mungu wetu kwa njia ya uimbaji. Wanahitaji sana maombi yako wewe na pia kuwaunga mkono pale DVD yao itakapotoka kwa kuinunua madukani.

Martha Mwaipaja
Rumafrica inawatakia mafanikio mema kwa hawa waimbaji, na pia inawapongeza waimbaji wote ambao wanapenda kufanya vitu vizuri kwaajili ya utukufu wa Mungu. Waimbaji wa sasa wameleta mapinduzi makubwa sana katika ubora wa Video zao. Mungu azidi kuwawezesha kupata fedha nyingi sana kwa kupitia huduma yao ili wazidi kufanya vitu vikali. Tukifanya vitu vikali vitaweza kuwavuta watu kwa Yesu kwani wataona kuna faida katika kumtumikia Mungu.

Beatrice Mwaipaja
Tulizoea ule wokovu ambao ulikuwa unatufundisha kuwa hatutakiwi kupendeza kwani ukipendeza utakuwa unatenda dhambi. Na hii ilisababisha watu wengi sana kutotamani wokovu na kutupa majina ya WALOKOLE NI WASHAMBA. Tunamshukuru sa Mungu ameweza kufuta hilo jina na sasa watu wanasema KUOKOKA NI FASHION hata kama wengine wanatafsiri tofauti, ila niseme kwa Yesu Kristo kunalipa na chenji inabaki. Okokeni sasa.
Tuone baadhi ya picha za uaandaji wa DVD hiyo inayokuja



Kulia ni Martha Mwaipaja na Beatrice Mwaipaja










Director Jackson akiwa kikazi




















Comments