RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EXCLUSIVE: FLORA MBASHA AKIFUNGUKA NA RUMAFRICA ONLINE TV JUU YA HISTORIA YAKE YA WOKOVU NA MAFANIKIO ALIYOPATA

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Flora Mbasha aliweza kufika katika ofisi ya Rumafrica na kuweza kuongea mengi juu ya tamasha lake la 14/06/2015 Ubungo Plaza Dar ambapo aliwaomba watu waweze kufika katika tamasha hilo kushuhudia uzinduzi wa DVD yake ya NIPE NGUVU ZA KUSHINDA na kutambulisha bendi yake ambayo atatumia kuimba LIVE.

Baada ya kumaliza mazungumzo hayo kama kawaida Rumafrica ilitaka kujua historia fupi ya maisha yake ya wokovu na faida alizopata tangia amempokea huyu Bwana wetu Yesu Kristo. Sasa Rumafrica imekusogezea hapoa ulipo usikie alichosema.

Flora Mbasha (kushoto) na mkurugenzi wa Rumafrica Rulea Sanga ndani ya Rumafrica Online TV

Na wewe ukitamani kufanya mahojiano juu ya huduma yako au biasha yako basi wasiliana nasi kwa simu +255 715 851 523 nasi tutarusha katika TV yetu ya Rumafrica Online TV.

Comments