RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIMBAJI BAHATI BUKUKU NDANI YA ARUSHA KUMUUNGA MKONO MGOMBEA URASI 2015 MH. EDWARD LOWASA

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Bahati Bukuku atakuwa Arusha kwaajili ya kumuunga mkono mgombea Urais 2015 Mh. Edward Lowasa. Rumafrica ikiongea na Katibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania kwa njia ya Watsap amesema, "Bahati Bukuku ametoa taarifa rasmi kwa uongozi wa CHAMUITA kuwa wakati wowote Bahati Bukuku ataelekea Arusha kwaajili ya kumuunga mkono Mh. Edward Lowasa katika harakati za kusaka Uraisi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015. Na sisi kama viongozi tumemuelewa na tunamtakia kila la heri katika safari yake na shughuli nzima ya kumuunga mkono Mh. Edward Lowasa".


Huu ndio ujumbe wa Katibu Mwenezi wa CHAMUITA, na aliweza kutuma picha akiwa na mwimbaji wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku, Rais wa CHAMUITA Addo Novemba na wengine aliokuwa nao.
Kutoka kushoto ni Rais wa CHAMUITA Addo Novemba, Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Bahati Bukuku, na Katibu Muenezi wa CHAMUITA Stella Joel



Comments