RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MARY MGOGO ANAKUKARIBISHA KWENYE TAMASHA LAKE UBUNGO PLAZA, KUTAKUWA NA RED CARPET

Watu wakiwa wamependeza kuja kumsifu Mungu katika tamasha la Mary Mgogo atakayekuwa akizidyua DVD yake ya MUNGU wa AJABU siku ya Jumapili hii pale UBUNGO PLAZA. Kutakuwa na kiingilio kwa wale watakaofika baada ya saa tisa, watalipia 5000 na wale watakaofika kuanzia saa 7 mchana hadi 9 mchana wataingia bure kabisa. Tamasha hili litakuwa na waimbaji wengi sana kama Bahati Bukuku, Atosha Kissava, MC Joshua Makondeko, Mc Bony Magupa, Manesa Sanga, Ibrahimu Sanga, Christina Mbilinyi, Daniel Safafri, Daniel Thomasi, Edson Mwasabwite na wengine wengi.

Mary Mgogo anakualika sana wewe mdau wa muziki wa Injili kufika katika tamasha lake, na kufika kwako ndiko kutasababisha tamasha kufana na kupendeza kwa utukufu wa Mungu. Siku hiyo kutakuwa na red carpet kama unavyoona hapo chini ambapo watu wataweza kupiga picha za kumbukumbu. Usikose ndugu yangu.


Comments