RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RISALA YA UZINDUZI WA FLORA MBASHA AKISOMWA NA MH. FREEMAN MBOWE ALIVYOZINDUA DVD YA NIPE NGUVU YA KUSHINDA

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Flora Mbasha siku ya Jumapili 14/06/2015 mida ya mchana ndani ya ukumbi wa kifahari wa Ubungo Plaza uliopo Dar es Salaam aliweza kuzindua DVD yake ya NIPE NGUVU YA KUSHINDA. Hii ni mara yake ya kwanza kufanya uzinduzi wa DVD zake zote alizoweza kutoa hapa jiji la Dar es Salaam. Flora Mbasha aliweza pia kutambulisha bendi yake ambayo atakuwa akiizunguka nayo mikoa yote ya Tanzania na nje ya Tanzania.

Msomaji wa Risala ya Flora Mbasha

Mh. Freema Mbowe alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hili ambalo lilidhaminiwa na The Fadhaget Sanitarium Clinic, Kidoti, ABE Sound, Wanawake LIVE, Gombo Tours, Clouds TV, Rumafrica na AG Press. Katika tamasha hili kulisomwa risala ambayo iliandikwa na kuchapishwa na Rumafrica ambao ni wataalamu wa kuandaa matamasha ya Kikristo Tanzania.

Risala hili ilikuwa inahitaji wadau wa muziki wa Flora Mbasha kumchangia fedha kwaajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki wake wa LIVE. Tunamshukuru sana kwani aliweza kuwatumia watu wake kumchangia Flora Mbasha robo ya yale malengo yake aliyoyaweka kufanikisha ununuzi wa vyombo vya muziki. Mh. Freeman Mbowe aliweza kumchangia kiasi cha 11,000,000 na usheee kufanikisha lengo lake. Huu ni moyo wa kipekee sana ambao Mh. Freeman Mbowe aliweza kuonyesha kwa Watanzania. Wakristo tunahitaji kuwa na moyo huu wa kusapoti kazi za watumishi wa Mungu iliwazidi kusonga mbele na kuwaleta watu kwa Yesu Kristo.


Rumafrica iliweza kupata baadhi ya matukio kipindi cha usomaji wa risala na zoezi zima la uzinduzi wa DVD. Tutazi kuwaletea matukio mengine. Ukihitaji mtu wa picha na video katika tamsha lako wasiliana na Rumafrica +255 715 851 523 tutakusaidia.Mungu awabariki sana.


 Flora Mbasha wa tatu kutoka kulia akisikiliza kwa makini Risala




Msomaji Risala akimkabidhi Mh. Freeman Mbowe Risala

KIPINDI CHA UZINDUZI WA DVD YA FLORA MBASHA
 Mh. Freema Mbowe akielekea jukwani kuzindua DVD ya Flora Mbasha
 Mh. Freeman Mbowe akipokea DVD kutoka kwa mhudumu
 Zoezi la ukataji wa DVD ukiendelea

BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KIDOGO KUSHOTO KUONA MUENDELEZO WA TUKIO HILI LA KIHISTORIA






 Mh Freeman Mbowe akisoma jina la albamu ya Frola Mbasha baada ya uzinduzi


 Flora Masha akiwa na Furaha baada ya DVD yake kuzinduliwa

KIPINDI CHA KUOMBEA DVD YA FLORA MBASHA BAADA YA KUKATWA UTEPE
 Mch. Maximillian akijiandaa kuiombea DVD ya Flora Mbasha
 Mch. Maximillian (kushoto) akiombea DVD ya Flora Mbasha

 Flora Mbasha akiwa katika maombi kuiombea DVD yake



KIPINDI CHA KUFANYA CHANGIZO NA MH. FREEMAN MBOWE KUSEMA JAMBO JUU YA TAMASHA HILI

Comments