RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA MWENGE: WANAOMNGOJEA BWANA



Rumafrica ilibata kibali mbele za Mungu cha kuweza kufika katika kanisa la Nabii na Mtume Josephate Mwingira la EFATHA lililoko Mwenge Dar es Salaam siku ya Jumapili ya tarehe 19/07/2015. Ibada ya pili ilianza saa 4 asubuhi na kumalizika saa 7 mchana ambapo Nabii na Mtume Josepahte Mwingira aliweza kuwaomba wachungaji wake watoe ujumbe wa Mungu kwa waumini na baadae aliweza kusimama na kuhubiri. Sasa naomba nikushirikishe mamchache kutoka kwa watuminishi wa Mungu.
Picha ya Nabii na Mtume Josephate Mwingira katika ibada za nyuma
WANAOMNGOJEA BWANA
Hao wanaomngojea Bwana watatiwa nguvu mpya na wataruka juu kama tai, mahali penye kupanda pana kushuka. Ukitaka kupanda unahitaji nguvu mpya, anayeshuka ana nguvu ya kushuka, mfano Yusufu alikuwa haeshimiki na ndugu zake lakini alikuwa na ndoto ya kuwa mtu wa juu, ndugu zake wakachukia kuwa Yusufu kupatiwa ndoto.
Yusufu alipitia changamoto nyingi sana, lakini haikumpa taabu kwani alijua yeye alioteshwa ndoto kuwa atakuwa juu, ndoto zako ulizonazo zitatimia.
Kanisa la Yesu Kristo alitanyamaza kimya, Kanisa likinyamaza basi Yesu amewakataa, nasi tunayemngojea Bwana tutapiga kelele na kumshukuru Mungu. Safari yetu tuliyonayo haina kituo hapa duniani bali kituo chetu kipo mbinguni basi.
HURUMA ZA MUNGU NA UPENDO WA MUNGU
Huu ni mwaka ulioamiwa kwa sababu huu ni mwaka wa kutembea na Mungu, na Mungu ametuhurumia, Efatha ni kituo kilicho salama.
Yesu alikuja kwa sababu ya kukutoa kwa shetani na kukuweka huru, tuliteswa na shetani na sasa tupo huru.
Zaburi 62: kwa sababu yetu sisi Bwana hatanyamaza, atahakikisha unabarikiwa, wana Efatha tumepata neema ya pekee kwa hiyo inatakiwa kuwaleta kwa Yesu ili waokoke. Mungu huko mbinguni hatulii kwa sababu yetu ili uwe huru, tunaomba Mungu mbingu isinyamaze kwaajili yetu.
Shetani, wachawi waache wafanye yao lakini hawataweza kwani neno la Mungu litatimia, tuachane na imani ya potofu ya kukatishana tamaa wana Efatha, watu wamezoea kumtumikia Mungu asiye hai. Tunaposema Mungu wa Efatha, tunamaanisha Mungu amesema nini na mbeba maono wa Efatha yaani Nabii na Mtume Josephate Elias Mwingira.
Kama ulikuwa unashindwa kushuhudia, pokea nguvu ya kushuhudia, tumepewa mamlaka ya matendo. Hutakiwi kuwa na mazoea ya kuzoea huduma ya Mungu, unatakiwa kunyenyekea na kutii.
UPENDO WA MUNGU
Methali 8:17, nawapenda wale wanipendao na wale wanitafutao kwa bidii wataniona, upendo ni nipe nikupe. Mungu atakupa yale unayoomba kama kama unampenda na atakuzidhishia, tunampenda Mungu kwa imani, kama humuoni Mungu basi unanafasi ya kuwapenda watumishi wake kwani hao wanatumiwa na Mungu kuleta Baraka zako kwako na pia kuleta ujumbe kutoka Kwake
.
Mungu ni Mungu anayetuwazia mema, Mungu tunampenda kwa kuwapenda watumishi wake kwani wao ni bomba lake la kupitisha ujumbe kwako. Kama unasema nampenda Mungu wa Efatha na ukawa humpendi mbeba maono wa Efatha basi wewe ni kichaa.
Upendo ni kumimina moyo wako kwa Mungu, Yohana 15:16 Sio sisi tuliyemchagua Yesu bali yeye ndiye aliyetuchagua. Matunda yakikaa kwetu basi tuombalo atatupa, Yesu ndiye aliyetutafuta na ndio maana leo hii unaenda Kanisani. Unapofika Kanisani na kufurahia uwepo wa Mungu, unatakiwa kwenda kuwatafuta watu wengine waje Kanisani na kumtumikia Mungu, unatakiwa kujiuliza katika wokovu wako umeleta wangapi kwa Yesu.
Kumpenda Mungu ni kupeda yale mahusiano yake.
WEWE MTU WA MAANA
Marko 7:54.
Kuna maneno sita yaliyotangulia kabla ya neno Efatha, lakini tuone haya matatu na mengine utasoma katika somo la MAANA hapo chini:
i.                     Akazama juu mbinguni, alikuwa anatafuta Mungu anamuonyeshe.
ii.                   Akawaambia watu, watu wanakuja Kanisani kwa kile tunachowaambia na sio tunavyowaona.
iii.                  Efatha maana yake funguka, mambo yako yanaanza kunyooka na kua mazuri.
Unapokuja Efatha unaona kila kitu kinakuwa cha maana, unatakiwa kunyoosha maana yako na usiponyoosha maana yako, wengine watanyoosha maana zao. Unachokifanya hakikisha maana yake inaonekana kila kitu unachofanya lazima kiwe cha maana. Kama mwana Efatha kila kitu kiwe cha maana. Ukijua maana unatoka gerezani na mambo yako yanaanza kuwa mazuri. Usifanye mchezo na mtu anayejua maana ya Efatha. Ukifanya ujinga utaona moto wake. Watu wenye maana hawarudi kwenye huzuni au ukame. Ukishaona umeanza kutengwa utambue umeshaanza kupata maana yako. Kuanzia sasa anza kuwatenga Watu/Marafiki wasiokua na maana katika maono yako. Chochote unachoona kinasababisha maana yako isitokee kemea mapepo hao. Sii unakua wa maana hapa duniani tu, bali hadi mbinguni. Mtu hawezi kuja kanisani bila ya kumtolea Mungu sadaka au zaka.
Ukiwa mtu wa maana unaenda kuamrisha adui zako. Mungu anasema atawaweka chini ya miguu yako.
Mungu akiamua kukudharau anakudharau kweli, anakuweka chini adui zako wanakwenda chini na anakwenda kuwaamrisha. Kuna watu wanakesha kwa mabaya kwako.
Sisi ni viumbe vipya ambavyo vinafanya mambo makuu ya Kimungu kwa watu wasiyoyapenda ya Mungu.
Kuanzia sasa:-
(i)                  Vaa kwa maana
(ii)                Cheza kwa maana
(iii)               Toa sadaka kwa maana
Fanya jambo lolote kwa maana.



Comments