Waimbaji wa nyimbo za Injili waliomo ndani ya Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) wamefanyika baraka kubwa kwa wakazi wa jiji la Mwanza kwa huduma yao ya uimbaji na maombezi. Chama hiki kiliamua kuongozana na Mch. Dkt. Rejoice Ndalima kuelekea Mwanza kwa lengo la kuliombea Taifa la Tanzania amani na utulivu wakiungana na wakazi wa jiji la Mwanza. Kama tunavyotambua kuwa nchi yetu ya Tanzania ipo katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, kwahiyo kama watumishi wa Mungu tunalazimika kukaa miguu pa Bwana na kumuomba Mungu wetu azidi kuipa amani nchi yetu ili yasitokee machafuko ya kivita na kuruga amani yetu.
Waimbaji hawa waliweza kupata muda wa kuwaombea wakazi wa Mwanza na kukemea mapepo yaliyokuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu. Hakika Mungu amekuwa mwema kwao, na nguvu za Mungu zilijidhihirisha kwa wananchi wa Mwanza.
Chama hiki kipo kwaajili ya kutetea haki za wanamukizi wa Injili Tanzania na pia kusaidiana wakati wa shida na raha. Na pia chama hiki kimesajiliwa na ni chama cha Kitaifa. Waimbaji hupata muda wa kufanya maombi kila mwisho wa mwezi na pia kufanya sifa kwaajili ya utukufu wa Mungu.
Wakazi wa Mwanza walionyesha upendo wa ajabu sana kwa wageni wao kwa kuwaandalia chakula na malazi bure kabisa. Kongamano hili lilileta msisimko mkubwa sana kwa wakazi wa Mwanza na hakika waliweza kujifunza kitu kwa waimbaji hawa kutoka Dar es Salaam na mkoa mbalimbali.
KIPINDI CHA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA MWANZA WAKIFANYA MAHOJIANO NA VIONGOZI WA CHAMUITA KUJUA MENGI KUHUSU CHAMA HICHO.
Kulia ni Ulimbaga Mwakatobe na kushoto ni Katibu Mwenezi Taifa Stella Joel
Mmoja wa viongozi wa CHAMUITA Magreth Sembuche akiwa na Ulimbaga Mwakatobe
Baadhi ya viongozi na wenyeji wa mkoa wa Mwanza wakihojiwa
Katubu Mwenezi wa CHAMUITA, Stella Joel
KIPINDI CHA MAOMBEZI NA UPONYAJI KIKIENDELEA
Madam Ruti (kulia) na Magreth Sembuche - wote ni waimbaji na viongozi wa CHAMUITA kutoka Dar es Salaam
Madam Ruti
KIPINDI CHA KUSIFU NA KUABUD
Ulimbaga Mwakatobe
Stela Joel kulia akiimba
Madam Ruti
Askofu Dkt. Rojice Ndalima kutoka Dar es Salaam (kushoto) akisikiliza Neno la Mungu akifutia Madam Ruti na Magreth Sembuche
BAADA YA KAZI NZITO YA BWANA ULIFIKA WAKATI WA KUPATA CHAKULA
Magreth Sembuche
Ulimbaga Mwakatobe
Stella Joel
Magreth Sembuche
KIPINDI CHA KURUDI DAR ES SALAAM KILIWADIA
Ulimbaga Mwakatobe akiwa kwenye ndege kurudi Dar akitokea Mwanza
ANGALIA MATUKIO MENGINE YALITOKEA JIJINI MWANZA NA WANACHAMUITA KWA KUBONYZA HAPA
ANGALIA MATUKIO MENGINE YALITOKEA JIJINI MWANZA NA WANACHAMUITA KWA KUBONYZA HAPA
Comments