MATUKIO YA TAMASHA LA MARY MGOGO NDANI YA UBUNGO PLAZA ALIVYOKUWA AKIZINDUA DVD YAKE YA MUNGU WA AJABU
Mary Mgogo kwa kabila ni Mkinga ambayo huduma yake ilianzia akiwa mdogo sana na baadae ikakakua na hivi sasa Mungu amempa kibali cha kuzindua DVD yake inayoenda kwa jina la Mungu wa Ajbau. Uzinduzi huu ulifanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi alikuwa Mh. Mkongoro Mahanga Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na pia ni Mbunge wa Segerea. Tamasha hili lilihudhuriwa na watu wengi sana ambao walikuja kwaajili ya kumtukuza Mungu wetu wa mbinguni.
Mary Mgogo
Hakika siku hiyo Mungu aliweza kugusa mioyo ya watu kupitia uimbaji wa Mary Mgogo na pia waimbaji wengine walioweza kuimba siku hiyo. Tamasha hili lilifanyika siku ya Jumapili 05/07/2015 ambapo kulikuwa na kiingilio cha sh. 5,000 kwa watu waliofika baada ya saa 9 mchana na wale waliofika kabla waliweza kuingia bure.
Mungu atabaki kuitwa Mungu, Mary Mgogo ambaye anaabudu kanisa la TAG aliweza kufanya vizuri sana katika tamasha lake na kusababisha ukumbi kuchangamka hasa pale aliposhusha nyimbo zake zenye upako wa kipekee. Hakika kazi ya Mungu itazidi kusonga mbele kwani wapo wenye nia ya kumtumikia Mungu. Mungu mbali na kumbariki Mary Mgogo bado anamtumia kwa njia ya uimbaji na yeye amekubali kumtumikia Mungu kwa njia hiyo.
Tuone baadhi ya matukio yalitokea katika tamasha hili. Rumafrica itazidi kukupa muendelezo wa tamasha hili...(Picha zimepigwa na Rumafrica +255 715 851 523)
Ibrahimu Sanga

Atosha Kissava
Atosha Kissava akiwa na Tumaini Njole (kulia)
ENDELEA KUFUATILIA BLOGU HII KUONA MATUKIO MENGINE KUHUSIANA NA TAMASHA HILI
Comments