RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MUENDELEZO WA MATUKIO YA UZINDUZI WA DVD YA MUNGU WA AJABU YA MARY MGOGO NDANI YA UBUNGO PLAZA JIJINI DAR ES SALAAM

Leo hii nitakupa baadhi ya picha za matukio ya uzinduzi wa DVD ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Mary Mgogo wakati akiingia ukumbini. Tamasha hili liliweza kukonga mioyo ya walio wengi kutokana na ubunifu alioweza kuonyesha mwimbaji huyo katika ukumbi huo wa kimataifa wa Ubungo Plaza.

Mary Mgogo alikuwa akizindua DVD yake ya MUNGU WA AJABU ikiwa ni DVD yake ya kwanza tangia ameanza kuimba nyimbo za Injili. Mwimbaji huyu ni muumini wa kanisa la TAG na amekuwa akimtumikia Mungu tangia utoto wake.

Mgeni rasmi wa tamasha hili alikuwa ni Naibu Waziri wa Ajira na Kazi Mh. Makongoro na ni Mbunge wa Segerea. Kulikuwa na waimbaji wengi sana ambao waliweza kumsindikiza mwimbaji mwenzao kama utakavyowaona katika tangazo hapo chini.

Tamasha lilifanyika siku ya Jumapili 05/07/2015 na lilianza saa 7 mchana ambapo watu 500 wa kwanza kuingia kuanzia saa 7mchana hadi saa 9 mchana waliweza kuingia bure. Wapambaji wa tamasha hili walikuwa Rumafrica na pia ndio waliojihusisha na shooting.

KIPINDI CHA MGENI RASMI KUINGIA UKUMBINI

  Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Ajira na Kazi Mh. Makongoro na ni Mbunge wa Segerea





 Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Ajira na Kazi Mh. Makongoro na ni Mbunge wa Segerea (wa pili kutoka kushoto)
 Mess Jacob Chengula (wa pili kutoka kulia)



KIPINDI CHA MARY MGOGO KUINGIA UKUMBINI
 Dancers wa Mary Mgogo Eno na Edo

 Wa pili kutoka kushoto aliyevalia nguo za kijani ni mtoto wa kwanza wa Mary Mgogo akiwa na wenzake wakiingia ukumbini

 Mary Mgogo akiingia ukumbini
 Mary Mgogo
 Mary Mgogo





Comments