RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KWAYA WA MLIMA WA MOTO ASSEMBLIES OF GOD YATOA UJUMBE WA MADHARA YA SIMU YA MKONONI KUPITIA NYIMBO


Katika ibada ya Jumapili 13/09/2015 moja ya kwaya ya Mlima wa Moto Assemblies of God Tanzania iliweza kutoa ujumbe wake wa madhara ya simu ya mkononi kwa watu waliokoka na jinsi gani ya kuepukana na matumizi hayo mabaya.

Askofu Mh. Dkt. Gertrude Rwakatare

Askofu Mh. Dkt. Gertrude Rwakatare aliweza kutoa Tshs. 200,000 kama pongezi kwa ujumbe huo waliouuimba, na ujumbe ulikuwa kama ifuatavyo, 
Simu ya mkononi imesababisha kuvunjika ndoa, wanafunzi wameacha masomo, kutokea kwa ajali, wa kuitenga Biblia na kutopenda kusoma Neno la Mungu,



Chakufanya sasa, ni kufungua macho na kuweza kuitumia vyema simu yako vizuri, kwasababu lengo la simu ya mkononi ni hurahisisha mawasiliano.

Hebu fikiria zamani tulikuwa tukiandika barua na tunasubiria wiki nzima barua kukufikia na tunakuwa na amani hata kama ujumbe ulikuwa unatufikia kwa kuchelewa sana.

Tunatambua kuwa simu hurahisha mawasiliano, lakini wapo watu wengine wanatumiwa na shetani kwa kupitia simu zao kwa kutuma ujumbe mbaya na matusi, kuvunja moyo, maneno ya kashfa n.k.

Lakini wewe mpendwa mtu wa Mungu tumia simu yako vizuri, kwatia watu moyo, kushuhudia, kuwakumbusha watu kuwahi ibada. Simu yako ifanyike Baraka kwa kuwaleta watu kwa Yesu, watu wamjue Mungu na Mungu atakubariki sana..Ameni

Askofu Dk. Gertrude Rwakatare alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na simu ya mkononi. “Simu imekuwa ni tatizo katika familia, ndoa, maofisi. Kuna baadi ya ofisi ukiingia tu unaona kuna kibao kinasema zima simu yako. Tunatmabua kuwa simu kazi yake kubwa sana ni kurahisisha mawasiliano na sio kuharibu. Tunatakiwa kuzitumia kwa heshima ili zitusaidie katika mawasiliano yetu kwa urahisi sana.
Kanisa lipo Tanzania, Dar es Salaam, Mikocheni B. Ukifika Mwenge panda bajaji au bodaboda zitakazokupeleka Mikocheni B kwa Mama Gertrude Rwakatare. Tembelea www.mountainoffiretanzania.blogspot.com








Comments