RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAMA ALIYEKUWA HAZAI (TASA) APATA WATOTO DOUBLE DOUBLE



Hakika hii ni siku ambayo Bwana ameifanya, Mungu amenikumbuka tena, Mungu wetu ni Mungu wa “tena”, ni Mungu wa “double double”. Niheshima zangu mbele ya kanisa na madhabahu hii takkatifu

kwa weli ninaiogoapa. Mungu wa Gertrude Rwakatare amenifuta machozi na amenitendea, amenifunika na aibu. Hakika Mungu yupo wapendwa, endeleeni kushikilia Imani na kumtafuta Mungu.

Ukisoma katika kitabu cha Kutoka 21:22 inasema, “Mjue sana Mungu upate kuwa na amani ndipo mema yatakapokuujia”. Ndugu wapendwa tung’ang’ane na huyo Mungu na tumaanishe na Mungu anajibu.

Nakumbuka mwaka jana (2014) nilikuwa mahali hapa nikiwa na mwanangu m

kwa kweli ninashindwa nimrudishie nini Mungu . Mungu kanitoa kwenye jina nililokuwa naitwa mwanamke tasa, na sasa nimekuwa mama wa watoto wawili. Mungu amenifanyia kicheko kwa muda wa mwaka mmoja nimepata watoto wawili na sio mapacha.

Ninapenda kumshukuru sana Mama Mh. Dkt. Gertrude Rwakatare popote ulipo natambua unanisikia kwa njia ya rohoni. Mama huyu aliniombea, alinitia moyo. Ninashukuru kwa kanisa zima kwa moyo wenu wa upendo.

Nisingekuwa katika kanisa hili la Mlima wa Moto sijui ningekuwaje, labda ningechanganyikiwa, lakini mama alizidi kunitia Moyo. Mama Gertrude Rwakatare alikuwa akisema pokea watoto wakati anahubiri, na mimi kwa imani nikawa napokea.

Kanisa la Mlima wa Moto linalipa, Mungu akijibu unapata double double na haijalishi unapitia kitu gani, wewe unapoambiwa pokea unatakiwa kupokea kwa imani.

Ninawashukuru wazee wa kanisa, wanamaombi,  mliweza kuniombea na kunitia moyo.

Unakaribishwa katika ibada zinazoendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God Mikocheni “B” kwa Askofu Dr. Gertrude Rwakatare lililopo Dar es Salaam – Tanzania.


Tembelea www.mountainoffiretanzania.blogspot.com au www.rumaafrica.blogspot.com




 

Comments