RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCH. NOAH LUKUMAYI: TUNATANGAZA VITA KATI YA ADUI SHETANI

Kutokana na Uchaguzi Mkuu wa Kitaifa kufanyika siku ya Jumapili 25.10.2015 Kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God liliamua kufanya ibada yake siku ya Jumamosi ili kuwaacha waumini wa kanisa hilo kuwa huru siku ya Jumapili kuwacgagua Raisi na viongozi wanaowataka.
Siku ya Jumamosi Askofu Msaidizi wa kanisa hili Mch. Noah Lukumai aliweza kutoa Neno la Mungu kwako wewe unayesona na kwa wale waliokuwepo katika ibada hii, na hivi ndivyo ilivyokuwa, " Ninaomba ufuatishe maneno haya, sema, “Katika Jina la Yesu, ninatangaza vita vya wapinzani, vianze kuachia katika jina la Yesu. Kila mpango wa shetani ambao unapingana na ibada hii sasa tunauharibu kwa jina la Yesu.
Kila roho ya mazoea tunakwenda kuiharibu kwa jina la Yesu. Kuanzia sasa moyo wangu na akilizangu zote zinakwenda kumtukuza Bwana. Kila Farao anayenifuatilia natangaza gharika, sunami, hatari juu yake kwa Jina la Yesu. Taarifa zoe mbaya zinazonifuata nikiwa kanisani leo ninaziahamisha kwa Jina la Yesu Kristo. Sasa ninakuomba useme, “Fireeeee” mara saba. Mungu akubariki sana….Amen.””
Tunakukaribisha kanisa kwetu Mlima wa Moto Assemblies of God, lililopo jijini Dar es Salaam, Mikocheni “B”. Ukifika Mwenge mataa waombe watu wa bajaji wakulete kanisa kwa mama Gertrude Rwakatare. Siku ya Jumapili kunakuwa na usafiri wa bure saa 2 asubuhi katika kituo cha Makumbusho au Mwenge Mataa.
Tembelea www.mountainoffiretanzania.blogspot.com au
www.rumaafrica.blogspot.com
Facebook kwa jina la Mountainoffire Tanzania.















Comments