RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WATU WAPATA CHAKULA CHA MCHANA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO SIKU YA "SUNDAY TO REMEMBER 2016"

Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" lililopo jijini Dar es Salaam, siku ya 31.01.2016 liliweza kuandaa chakula kwa waumini wote na wageni waliofika katika ibada ya JUMAPILI YA KUKUMBUKWA (Sunday to Remember). Ibada hii ilianza saa 12 asubuhi na kumalizika saa 12 jioni, watu waliweza kupata Neno la Mungu na pia waliweza kupakwa mafuta ya upako na kugawiwa maji ya upako pamoja na kalamu za upako.

Kanisa hili ni moja ya makanisa makubwa sanaTanzania ambalo likuwa mstari wa mbele sana kuwasaidia Watanzania katikamaswala ya kiimani na pia kuwasidia kuwainua kiuchumi. Ni moja ya makanisa ambayo yamefanikiwa sana na kuwa na waumini weni sana. Kanisa hili ni kanisa linaloongozwa na mama ambaye amekuwa akifanya jitihada zote kuhakikisha kanisa linazidi kuwainua watu wazidi kumuamini Mungu ili siku ya mwisho wakamuone Mungu juu mbinguni.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ambaye ndiye kiongozi wa kanisa hili aliweza kuwashukuru wamuni wa kanisa hilo kwa kufika kwao na kutii sauti iliyotolewa madhabahuni ya kuwataka watu wafike kanisani saa kumi na mbili alfajiri.

Kama  Watanzania na watu wote wanaompenda mtumishi huyu tuna kila sababu ya kumuombea ili azidi kumtumikia Mungu na watu wakaokolewe. Munguibariki Tanzania, libariki kanisa la Mlima waMoto, Mbariki Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

KIPINDI CHA MAANDALIZI YA CHAKULA

Mtumishi Prisca (kulia) akiwa na baadhi ya waumini wakisubiri chakula kuiva

 CHAKULA KIKIPELEKWA KANISANI


KIPINDI CHA KUGAWA CHAKULA

 







 
BONYEZA "Read More" HAPO CHINI KUONA MATUKIO MENGINE






























Comments