MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

ALIYEKUWA MGANGA WA KIENYEJI KASIMU SELEMANI ABATIZWA NA WAKAZI WA KIZANI GEZAULOLE KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

Baada ya mkutano wa Injili wa siku 8 kumalizika katika viwanja vya kanisa jipya la Mlima wa Moto  Kizani Gezaulole Kigamboni jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili 28/02/2016 ambapo wiki iliyofuata kulifanyika Semina kubwa ya nje katika viwanja hivyo hivyo na kumalizika siku ya Jumapili 06/03/2016. Semina na Mkutano huo ulifanyika baraka kwa wakazi hao na kusababisha watu wengi kuokoka na siku ya Jumapili 06/03/2016 waokovu wapya wa Kizani Gezaulole na sehemu za jirani waliweza kubatizwa Ubatizo wa maji mengi na wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" katika beach ya Gezaulole Kigamboni.

Kasimu Salum Selemani aliyetaka kumgandisha jukwani Bishop Dr. Getrude Rwakatare asisimame kuhubiri naye aliweza kubatizwa siku hiyo. Watu walikuwa ni wengi sana, na wengi waliguswa na nguvu za Mungu, na walimshukuru sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kuweza kusogeza huduma hiyo karibu na makazi yao kwani kwa muda mrefu wameteswa na nguvu za giza, wachawi na waganga. Tuone jinsi zoezi la kubatiza lilivyokuwa kwa njia ya picha.
Mzee wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Nyatco na Cameraman wa Mlima wa Moto Stanley Ndenga wakibadilishana mawazo katika eneo la ubatizo
 Wakisubiri kubatizwa

 Kasimu akielekea kubatizwa
 Kasimu Selemani akibatizwa na watumishi wa Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B"
 Kasimu akitoka baharini baada ya kubatizwa
 Mch. Kyando wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" (kulia) akiwa na Kasimu Selemani
 Mwekahazina wa Vijana Mlima wa Moto Mikocheni "B" (kulia) Vctor akiwa na Kasimu baada ya kubatizwa
 Waliobatizwa wakirudishwa kanisani kwa seminaBONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KUONA MATUKIO MENGINE


0