MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

GWT WAKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI JUU YA TAMASHA LAO LA UPENDO FESTIVAL LITAKALOFANYIKA LEADERS-PASAKA


Kutoka kushoto ni msemaji wa tamasha hilo, Emmanuel Mabisa, Shaweji Somba na Isaack Didas ambao ni wajumbe.
Viongozi hao wakitoa ufafanuzi wa jambo...Mkutano ukiendelea.

Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili watakaotumbuiza siku hiyo, Levy Ngoy (kushoto) na Josiah Sadock (katikati).

Wanahabari wakichukua tukio hilo katika Hoteli ya The Atriums ulipofanyika mkutano huo.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kampuni ya Legendary Music entertainment tumeandaa tamasha la pasaka litakalofanyika jumapili ya pasaka tarehe 27.03.2016, katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaam kuanzia saa 10: 00 asubuhi mpaka saaTano kamili Usiku. Nia na lengo la kuandaa Tamasha hili ni kuwakusanya pamoja wakristo wote ili waweze kumsifu Mungu na kufurahia kwa pamoja sikukuu ya Pasaka pasipokujali dhehebu, jinsia na Umri .

Kutakuwa na burudani kutoka kwa waimbaji na wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili pamoja na Bonanza la michezo kwa mpira wa miguu, na michezo mbalimbali na zawadi zitatolewa kwa washindi watakaopatikana. kutakuwa na Nyama choma, Vinywaji na Vyakula vya kilaaina.

Wasanii wa Nyimbo za Injili watakaoshiriki katika tamasha ni pamoja na Ambwene Mwasongwe, Faraja Ntaboba, Grolious worship team, Edson Mwasabwite, Sarah Shila, Emanuel Mbasha, Upendo Kihaile, The Joshoua Generation, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, kkkt kimara, Angel Bernard, Calvary Band, Tumaini shangilieni Choir kutoka Arusha, Chang’ombe Vijana kwaya, The Next Level, Doxers praise Team, MiseRecordians, Angel Magoti, Fridah Felix, The Voice, na wengineo wengi.

(Na Denis Mtima/Gpl)
0