RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KUWAANGANIZA MAADUI ZETU - BISHOP Dr. GERTRUDE RWAKATARE WA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 20.03.2016 katika ibada ya kufunguliwa, aliweza kutoa ujumbe wa kuwaangamiza maadui zetu kama Herode alivyoangamizwa ikiwa ni sehemu tu ya mahubiri aliyohubiri siku hiyo. Tusome kile alichohubiri, karibu.

Nachotaka kukuambia ni kwamba wewe hukuzaliwa hivyo ulivyo, huo haukuwa mpango wa Mungu. Mungu alikupanga uwe mtawala, Mungu alikupanga uwe bilionea, Mungu alikupanga uwe na mume wako na mke wako. Lakini upo mahali ulipo kwasababu ya watu wabaya wanatamani kukuangusha.
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

katika maisha unapoishi lazima ufike mahali ujiulize, kama ni kushindwa kwanini wewe ushindwe na sio wengine washindwe. Ni kweli unaweza kusema ninashindwa kufanikiwa, lakini jiulize kwanini mimi (why me and not others?). Nimejaribu kwa uwezo wangu wote sasa kwanini siinuki?, kwanini sifanikiwi?, kwanini siendelee mbele? kwanini maisha yangu yamekuwa kiwete? Kwani haya yote yanatokea wakati ninauwezo, ninaamumka saa 11 asubuhi ninaenda kazini narudi usiku na nina lala na viatu lakini sioni mafanikio!
Katibu wa kanisa la Mlima wa Moto Mr. Kibona (kulia)

Mimi nimekuwa ni kiwete kiuchumi. Hakuna jambo langu ninapanga nikafanikiwa. Kulipa kodi ya nyumba ni kesi, kulipa ada ya shule ni kesi, kula chakula ni shida, vaa yangu ni taabu.

Watu wengi tu vilema, ujue kuna mtu anakuvuta nyuma kiroho usiende mbele, unapenda kwenda mbele lakini unashindwa kwasababu yuko mtu mmbaya anakuvuta. Unajiona wewe maisha yako yako hafifu, valuvalu. Unatakiwa kujiuliza kuwa hivi kweli umeokoka? Waliokoka hawaoko hivyo!!. Unajikuta maombi yako yako shagalabagala huombi kwa kumaanisha, Jumapili unakuja kanisani saa tano asubuhi badala ya kuja mapema. Kanisa limekuwa kituo cha polisi, ukiona hivyo ujue wewe ni kiwete wa Kiroho.
Utakua mtu amekuangusha na wewe unakata tamaa ya kumtumikia Mungu. 
Leo tunasimama mbele za maadui zetu na Mungu wetu. Kila mtu aliyesimama kuchangia anguko lako, na yeye akaanguke kwa jina la Yesu, kila mtu aliyechangia kuangusha ndoa yako na mahusiano yako na mchumba wako, leo tunamrudishia yeye kwa jina la Yesu.
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Leo ni siku yako ya Return to Center. Mtu aliyesababisha kazini kwako usiinuke (wenzako wamepata vyeo wewe unaachwa kwasababu yuko mtu anaficha file, anachongea, anasema maneno), leo ndio siku ya kung'oa Herode aliyesimama kinyume chako ili uweze kufa. Kazini kwako watu wanakuchukia kwasababu yuko Herode. Ule mchango ulioingia kwa Herode akafa, leo ninaachilia mchango wa kifo uende kwa adui yako kwa Jina la Yesu.
Wazee wa kanisa la Mlima wa Moto

Kuna mtu amekuweka mahali fulani (ameku-fix). Ukimchunga mbuzi na ukimfunga anakwenda sawasawa na kamba, na wewe wamekufunga kama mbuzi. Wako watu wana-remote maisha yako, wanaharibu maisha yako, una[potaka kwenda mbele anakurudisha, unapotaka kufanikiwa anakurudisha, unakaribia kushika mafanikio yako yeye anakurudisha, umekuwa ni mtu wa mahangaiko. Leo ni mwisho wa kuhangaishwa kwa jina la Yesu.
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
kila mchawi aliyeinuka kukufunga kamba usiende mbele, leo tunaagiza moto wa mbinguni, uweze kushuka na umteteketeze kwa jina la Yesu. "Enough is Enough". Shetani anakuonea kwasababu huendi kwa mganga, huna fundi, huna babu, uko mwenyewe, maombi yako hafifu, na adui yako anasema, hapahapa huyu ndio namuweza. Lakini mimi ninakuambia, "Penye mchawi kuna Mungu", "Kwenye adui kuna Jeshi la Malaika", tutalituma liende lilkaangamize. 
Leo tunaachilia mtu mkorofi amkalie na amfunge shingoni, amefunge kwa mitalimbo katika jina la Yesu, ammpe misukosuko katika jina la Yesu. Roho ya vifo, roho ya misiba tunaachilia kwa maadui zako kwa Jina la Yesu. Kama hao maadui hawafi wao basi wafe wajukuu zao na watoto wao.

Bwana Yesu asifiwe, umeonewa sasa imetosha, leo Mungu ameingilia kati anataka abadileshe kibao. Naomba usimame mahali ulipo. Sijui una Herode gani anayekusengenya, sijui una adui gani anayekuonea, sijui una nani anaye anayesimama nyuma yako na kusema lazima nihakikishe unaanguka.
Wako watu kazi yao ni kuvunja heshima ya watu. Utaona mtu alikuwa na heshima yake na sasa inashuka chini. Ndani ya kanisa watu tumeokoka, lakini mtu anamuona dada mzuri anajilinda anaanza kusema, "Yule ni Malaya" sasa unaposema hayo Je, uliniona nikifanya uzinzi? kwanini hukunikamata ugoni. Unaposema hivyo maana yake unataka waokoke wabaya wa sura na sio warembo kuokoka! Akiokoka mrembo unaanza kusema, "Muaangalie huyu katoka guest". Je, uliniona guest?, kwanini hukunikamata?  Nikuogope wewe ni nani, kama ninafanya si ninafanya tu, kwani utanifanya nini..!! Nikiamua kuolewa na mdunia si naolewa tu kwani uatanifanya nini..!! Kwasababu nimependa mwenyewe kuokoka kwangu nitaulinda ushuhuda.
Kuna faida gani kukaa kanisani? Kama unakuja kanisani halafu unachafua nafsi yangu, unanivunja moyo nisiende mbele, mambo ambayo niliacha miaka ya nyuma unafufua sasa ili iweje..!! Ninakuambia niache, waacheni wasichana wazuri waacheni, acheni kusema sema maneno. Hakuna mtu anapenda kukaa peke yake. Sasa mwanaume anapokuja anasema nimekupenda, mimi nifanyeje? Unataka nikakamate wanaume kwa nguvu waniue.
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Leo tunaachile mchango uliomuua Herode kwa adui zetu kwa jina la Yesu. Muulize mama yako, jirani yako, ni nani kakuangusha ukavunjika miguu, ukajikuta kiwete. Mungu anaweza kukupanga uwe mtu wa maana, uwe supporter wa kanisa, lakini yuko yahaya unayemjua wewe anaharibu mambo yako hayaendi sawa. Lakini tunasemaJeshi la Malaika linalotutumikia litaenda likawachape viboko katika jina la Yesu, wakacharazwe viboko katika jina la Yesu
Mtu anayepanga kukuharibia huyu ni muuwaji, mtu anayepanga mambo yako yasinyooke huyu ni muuwaji. Kwasababu tupo kanisani lazima tuite moto uteteketezao uweze kuteketeza maadui zetu, lazima tuagize Roho za misukosuko ziwakalie kooni maadui zetu. Yeye anayetarajia wewe yakupate yampate yeye mara kumi kwa Jina la Yesu, afukuzwe kama mpwa koko, yeye na umbea wake watu wamteme mate puuuuuu. "You are suppose to be a boss", You are supoose to somebody's wife. Unakuta umeachwa solemba, kila mchumba yuko yahaya. Tunakemea kwa jina la Yesu

Comments