Select Menu

News

UBUNGE

UBUNGE

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

JIFUNZE KIFARANSA

JIFUNZE KIFARANSA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

» »Unlabelled » MAREHEMU MWALIMU FURAHA ALIYEWAKINGA WAKRISTO KUTOKA KWA AL SHABAB ATUZWA


Sanga Rulea 11:11 AM 0


Marehemu mwalimu aliyepigwa risasi akiwakinga wakristo wasiuawe na magaidi wa Al Shabab ametuzwa medali ya juu zaidi na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Rais Kenyatta alipokuwa akihutubia taifa alisema kuwa wale wakenya wachache wanaoonesha ujasiri wa kukabiliana dhidi ya al shabab watatuzwa.
Rais Kenyatta alihutubia taifaNa hivyo akasema kuwa Mwalimu Farah ametuzwa heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi.Marehemu Salah Farah alikuwa katika basi lililokuwa likiwasafirisha abiria kutoka mji mkuu wa Nairobi kuelekea Mandera walipotekwa na wapiganaji wa Al shabab

Punde wapiganaji hao wakaanza kuwagawanya waislamu na wale wasio waislamu.
Hapo ndipo Mwalimu Farah na abiria wengine waislamu waliponga'amua nia ya wapiganaji hao ilikuwa ni kuua wakristu , waliibua mbinu ya kuwakinga abiria wakristo miongoni mwao ilikuokoa maisha yao.
Farah na wenzake wawili walijeruhiwa vibaya baada ya kukataa kugawanywa kwa makundi.
Kwa bahati mbata Mwalimu Farah alifariki mwezi Januari baada ya kuuguza majeraha ya risasi kwa takriban mwezi mmoja.
Tukio hilo la kijasiri lilichochea umoja miongoni mwa wakenya ambao wameshambuliwa mara kadhaa na magaidi wa Al Shabab.
Hiyo ilikuwa ni mara ya pili basi la kampuni hiyo ya Makkah kutekwa.
Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa waislamu.
Kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili mwaka uliopita lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa.
Source:bbcswahili

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS