MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MEGA MKATE NA PRAISE POWER RADIO NDIO STORY YA MJINI KWA SASA..!!!

Ukiwa wewe ni mdau na mkereketwa wa kazi ya BWANA basi hutaweza kutuangusha siku ya Jumapili ya Pasaka ya tar. 27.03.2016  saa 7 mchana wakati watangazaji wa Praise Power Radio watakavyokuwa wakimega mkate special ulioandaliwa na Praise Power Radio ndani ya ukumbi wa Urafiki Social Hall Sinza Lego. Utakuwa unajiiuliza kumega mkate kuna maanisha nini? Hili ni fumbo ambalo siku hiyo kwako itakuwa surprise utakapoona watangazaji hawa wakimega mkate.

Event hii imewashirikisha waimbaji wengi sana kama utakavyowaona katika poster hapo chini. Lengo kubwa ni kusherekea siku ya Pasaka na kuweza kubadilishana mawazo na watangazaji wako ambao umekuwa ukisikia tu sauti zao bila hata kuwaona LIVE.

Siku hiyo mambo yote yatakuwa LIVE, kutakuwa na bendi zitakazokuwa zinapiga LIVE na pia utapata kuona yale MAAJABU YA DUNIA ambayo mtangazaji wa PPR Emmanuel amekuwa akitangaza sana katika kipindi chake cha MAAJABU ya dunia. Utaweza kuona katika luninga ambayo itakuwepo ukumbini.

Siku hiyo ni siku ya kufurahi na kuruka kwa BWANA na sio siku ya majonzi. Shida zetu tutaziacha majumbani mwetu na tukirudi majumbani shida zote zitakuwa zimeisha na zimetoweka katika nyumba zetu kwasababu utarudi na upako wa ajabu na amani katika nyumba yako.

Usikose mtu wangu kufika mahali hapo, si unajua tena kuwa Mungu wetu ni Mungu wa sifa, kwahiyo siku hiyo imetengwa special kwa kumsifu Mungu wetu na kumega mkate na Praise Power.

Basi soma hilo tangazo kuona mambo yatakavyokuwa.

0