MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MISS UBUNGO AWAPA ZAWADI YA PASAKA WATOTO YATIMA

Miss Ubungo 2014, Diana Joachim (kulia) akimkabidhi zawadi mtoto Anitha Constantine ambaye anayeishi katika Kituo cha Chakuwama- Sinza.

Watoto wanaoishi kwenye kituo hicho cha kulelea yatima wakiwa katika picha.
Baadhi ya zawadi alizozitoa.

MISS Ubungo 2014, Diana Joachim Kato, jana aliwapa zawadi ya Pasaka ya vyakula na vinywaji watoto yatima wa Kituo cha Kulelea Yatima ‘Chakuwama’ kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam.

Zawadi hizo zilikabidhiwa kwa katibu mtendaji wa kituo hicho, Hassan Hamis ambaye alimshukuru kwa msaada wake kwa kuwakumbuka watoto yatima kusherehekea Sikukuu ya Pasaka pamoja nao.

Mrembo huyo alisema kuwa lengo kubwa la kwenda kutoa zawadi hizo ni namna alivyoguswa na moyo wake wa kusherehekea Sikukuu ya Pasaka na watoto hao ikiwa ni kuwatia moyo ili waweze kuishi katika maisha ya furaha.

“Nimeamua kuja kutoa zawadi hizi japo kidogo lakini kwa Mungu ni kubwa hasa nikiangalia siku ya leo ni siku ya furaha na kidogo nilichonacho nimependa niwape zawadi wafurahie sikukuu hii,” alisema Diana.
0