RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SHUHUDA KUTOKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA

SHUHUDA ZA JUMAPILI 10.01.2016
MAPANYA YALIYOKULA NDOO ZOTE NA VIATU YATOWEKA
Nyumbani kwangu kulikuwa ana panya wengi sana, kuna siku nimerudi nikakuta wametoboa ndoo zote ndani, nikachukua viatu nikavificha kwenye ndoo kubwa nikafunika baada ya muda nikakuta viatu vyote vimeliwa, ila nguo za mume wangu huwa hawagusi hua wanakimbilia za kwangu too, vitu vingi wamevunja vifaa vya maabara vya gharama wamevunja, nikamwambia mama ibada ya jumatano usiku, mama akaniambia ukirudi nyumbani hutaona panya tena na kweli niliporudi sikuona panya tena

MUME WAKE APATA FEDHA NYIMGI NA SHAMBA LAKE LALILMWA

Nilinunua sticker nikasema nataka kujiajiri, nilikuwa na wenzangu wawili tukaenda kukodi mashamba ya kulima tukalipia ili watulimie, jana tukawa tunaenda kukagua kama wameshalima, tukakuta hawajalima kwa wenzangu lakini kwangu nikakuta wameshalima kote kabisa Mungu wa Nabii Flora kafanya, lakini pia toka tumechukua hii sticker, mume wangu huwa anaondoka nayo anaweka kwenye vest, sticker imemsaidia sana, wiki nzima amekuwa akipata pesa kazini nyingi sana

SHUHUDA ZA JUMAPILI 07.01.2016

Unajua kilichotokea ni kwamba huyu kaka tumezunguka kwa muda wa mwaka mmoja na miezi sita tumempeleka katika hospitali nyingi huku na huko mpaka Muhimbili, mwisho wakatueleza kwamba ana kansa ya koo na kwamba imeshaenea mpaka kwenye kichwa na imesambaa mpaka mwili mzima, kwa hio inabidi waanze kumpiga mionzi, mimi nikakataa wasianze kumchoma mionzi kwa sababu wakishaanza kumchoma mionzi maana yake wamemmaliza kabisa, sasa tukapata wenzetu wakatuelekeza kwamba kuna Nabii mkienda manaweza mkapata maombezi na hilo tatizo likawa limekwisha, tukaja hapa kama wiki mija ilyopita, kwa kweli alitupokea vizuri na akaweza kutuombea na hilo tatizo likawa limekwisha, lakini alipotuombea wakati tunatoka hapa kitu cha ajabu, tulishangaa na tulicheka sana, tumefika kwenye banda hapo juu akaomba yeye mwenyewe chungwa, akala lile chungwa lote akamaliza na hakukohoa kabisa, halafu tulikuwa tumebeba uji kwenye thermos akanywa akamaliza na hakukohoa kabisa, na tulifiika nyumbani salama kabisa kwa sababu alikuwa anatapikaga njiani zamani, akafika akatulia na nyumbani kulikuwa na mapaka wanatembea kwenye paa juu lakini pia tulilala salama bila kelele za paka wala panya mpaka leo. 0018 na sasa hivi anakula kidogo kidogo na uji anakunywa.

Tembele: www.nabiiflora.blogspo.com
www.facebook.com/Nabii Flora Peter
Youtube: Nabii Flora Peter

Comments