MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

NABII JOSEPHATE MWINGIRA KATIKA IBADA YA JUMAPILI 24/05/205


IBADA KUU TAREHE 24/05/2015 EFATHA MWENGE.

Baadhi ya mamia ya wana EFATHA walioudhuria Ibada ya kwanza Efatha MInistry, Mwenge Dar es Salaam-Tanzania. Nawe ungana na wana wa MUNGU Ukusanyike pamoja na Waabuduo, Kumwabudu MUNGU wetu MKUU
USHUHUDA: "BWANA wetu YESU KRISTO YU HAI"
APATA SIKU ZAKE ZA HEDHI BAADA YA KUKAA MIAKA MINNE.
Naitwa Magdalena, Napenda Kumshukuru MUNGU ilikuwa ni siku ya Jumamosi siku ya Uji hapa Kanisani, Mimi nilichaguliwa kwenda Kupika uji, baada ya kupika Uji na kunywa Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii akatoa Unabii akasema, Yeyote aliyekuwa na Ugonjwa unaishia Getini, na Akasema kuwa kuna mtu ambaye Hazioni siku zake yapata miaka minne sasa anakwenda kuziona, Mimi nililichukua lile neno kwani lilikuwa la kwangu.

Siku ya tarehe 17 nilipofika Nyumbani Usiku nilishangaa sana Niliziona siku zangu NILIFURAHI sana, NAMTUKUZA MUNGU kwa hili.
Pia nimeleta Zawadi za Shukrani kwa Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Mama Eliakunda Mwingira, Mchungaji David Mwakisole na Elibariki Urasa.
Namshukuru MUNGU kwa Kunipa Kibali KUSHUHUDIA kile Alichonitendea. Wewe ambaye bado Hujapokea Muujiza wako, USIKATE TAMAA, Mimi nilikuwa nakuja Ibadani kila Jumapili kwa Miaka minne lakini tarehe 17 ndiyo ilikuwa SIKU Yangu, na Wewe siku yako Ipo, Nenda kwenye UWEPO wa BWANA kila Wanapokusanyika Watakatifu, MARUFUKU Kukata Tamaa.


USHUHUDA: "BWANA wetu YESU KRISTO YU HAI"
MAGONJWA BASI,.....
Naitwa Wiston David namshukuru Mungu kwa neema ya Wokovu ambayo ninayo mimi, sababu kabla Sijaokoka nilikuwa nasumbuliwa na magonjwa ya kila mara, haipiti wiki mimi ninaumwa, ila baada ya kufika hapa Efatha na kufuata maagizo ya Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, ile hali imeondoka na tangu nilipo OKOKA mpaka leo yapata Miaka Mitano SIJAUGUA tena, Namshukuru MUNGU sana. Pia mimi nilikuwa mfanyabiashara ila kila nikipata Faida Pesa ilikuwa inanikimbia kabisa, ila baada ya kufika hapa EFATHA, sasa Biashara yangu inaenda vizuri na FAIDA Naiona.

Siku moja nilienda Kibaha kufanya kazi ya BWANA, na Mimi nilikuwa natamani kufungua Shule ya Nursery. Baada ya kufanya kazi ya BWANA nilipata mtu akanipa eneo na sasa nimefungua Shule yangu na inaendelea vizuri. Yamkini wewe unateseka na magonjwa njoo EFATHA Utapona maana kuna NGUVU ya MUNGU, mimi Nimemuona.

Posted by EFATHA MINIS