RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PAPA WEMBA AANGUKA JUKWANI NA KUFARIKI

Hakika duniani ni wapitaji, hakuna anayejua kesho yake a dakika moja iliyo mbele yake. Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu na kuwa na ile hofu ya Mungu. Tufanye kazi ya Mungu kwani hatujui lililo mbele yetu. Leo hii imemtokea Papa Wemba mwana muziki maarufu sana duniani, hatujui dakika ya baadae litamtokea nani.

Sasa imeripotiwa na mitandao mbalimbali ya Afrika kwamba Mwimbaji huyu mkongwe Papa Wemba kutokea Congo DRC amefariki muda mfupi baada ya kuanguka ghalfa akiwa anatumbuiza jukwaani nchini Ivory Coast kwenye tamasha aliloalikwa kutumbuiza.

Habari hii ni kutoka kwenye moja ya mitandao ya kuaminika nchini Congo DRC lakini Rumafrica inaendelea kufatilia kwa karibu kujua ukweli na mengine zaidi ya Papa Wemba ambaye inaripotiwa amefariki akiwa na umri wa miaka 66.

Hii video fupi hapa chini inaonyesha sekunde za mwisho akiwa jukwaani na kuanguka

VIDEO CLIP ALIVYOANGUKA

Comments