RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RASMI KILA JUMAMOSI HIKI NDIO KITAKUWA KINAFANYIKA DAR ES SALAAM




Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli, tangu iingie madarakani moja ya ajenda ambayo imekuwa ikisisitizwa ni kuweka mazingira safi ambapo, Rais Magufuli mwenyewe aliongoza kampeni hiyo na kampeni hiyo imeendelezwa na watendaji wengine wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

April 30 2016 viongozi mbalimbali, wasanii na wananchi walifanya usafi maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na baadae kufanya matembezi kutoka maeneo ya Ilala, Temeke na Kinondoni na kukutana Leaders Club ambako imezinduliwa rasmi kampeni ya siku 90 ya Dar es salaam kuwa safi.

Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda ameizindua kampeni hiyo na amezungumza haya……..

>>>’tuliacha nafasi ya 2015 na kurudi nyuma kwamba kila mmoja atafanya usafi kwa sababu anajua ni wajibu wake lakini kwa kuwa tumeshindwa kutumia fursa hiyo sasa acha tufanye usafi kwa kushurutishwa na mamlaka tuliyopewa na Rais’

>>>’kamanda Sirro anajua kwamba amri yangu ni utekelezaji sitaki kuona biashara ya daladala inapitapita hapa mjini siku ya jumamosi nataka kuona usafi unafanyika na baada ya pale saa 3 tutafanya biashara zetu‘;-Paul Makonda

Aidha Paul Makonda amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuunda kamati ili kuchunguza makampuni ya usafi kama yapo yanayomilikiwa na watumishi wa umma kwa sababu inakiuka sheria ya utumishi wa umma…….

>>>’tunao watumishi wa umma wameanzisha makampuni ya kusafisha miji yetu lakini kwa kwa mujibu wa maadili ya utumishi wa umma kuna kipengele cha mgongano wa maslahi kwa hiyo RAS ninakuagiza ukatangaze Kamati itakayochunguza makampuni yote‘

>>>’zaidi nataka hiyo kamati iende kuangalie makampuni haya yanayoshinda tenda mengi hayana vifaa kama yalivyoeleza kwenye makaratasi yao:-Paul Makonda