MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

WATU WAZIDI KUBATIZWA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI SIKU YA JUMAPILI 03.04.2016

Tuna kila sababu ya kusema asante Bwana wetu Yesu Kristo kwa kazi unayofanya katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tunaona mkono wako ikiwagusa watu wako wanaotii sauti yako na kufuata yale unayotaka wayafuate kupitia kitabu chako kitakatifu yaani Biblia. Tumeona ukifungu milango ya mafanikio katika maisha yetu na sasa tunafurahia wokovu tuliopata.
Nje kidogo ya kanisa la Mlima wa Moto. Waumini wapya wakielekea kwenye basi tayari kwa safari ya kwenda baharini kubatizwa

Siku ya Jumapili 03.04.2016 watu waliweza kubatizwa baada ya kuongozwa sala ya toba na mch. Elizabeth wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni. Wachungaji na wazee wa kanisa la Mlima wa Moto waliweza kuwaombea na baadae kitengo cha watumishi wa Mungu ambayo wamefanyika baraka kubwa sana katika kanisa la Mlima wa Moto kwa kuwabatiza watu wengi sana, waliweza kuwapeleka baharini kubatizwa.
Basi la kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" lilisubiria waumini wapya tayari kwa safari ya kuelekea baharini kubatizwa
Wakiwa baharini, waliweza kupokea Roho Mtakatifu baada ya kuzamishwa katika maji. Hakika Mungu alikuwa upande wao. Watu hawa kwa sasa wamekuwa viumbe wapya na sasa wanajiunga na darasa kupata mafundisho ya kukulia wokovu.
Sasa ambaye bado hujabatizwa, ni wakati wako sasa wa kujiunga na kanisa hili ili tuweze kukubatiza, kwani hata Bwana wetu Yesu Kristo alibatizwa kwa maji mengi, iweje wewe..!!!..Mungu akusaidie upate hamu ya kuokoka na kuishi maisha ya wokovu. Watumishi wa Mungu wako tayari kukubatiza ili ufanyike kiumbe kipya na siku ya mwisho ukaonane na Mungu mbinguni. Mungu akubariki sana. Ibada zetu zinaanza saa 3 asubuhi. 

0