MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

08.05.2016: KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" LAFANYA IBADA YA KUWAOMBEA AKINA MAMA KATIKA SIKU YA WAMAMA ULIMWENGUNI

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na kanisa zima la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 08.05.2016 lilifanya ibada maalum kwaajili ya kuwaombea wamama wote duniani na pia kumshukuru Mungu kwa kuwapa uvumilivu wamama katika mapito wanayopitia katika maisha yao. Ibada ilihudhuriwa na watu wengi sana ambao walifika kwaajili ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayozidi kuyafanya kwa wamama duniani.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliwaomba watu kuwakumbuka mama zetu kwa mavazi, chakula, malazi au  kwa kitu chochote tulichobarikiwa nacho. Pia alisistiza juu ya Mahusiano mazuri (Petro 1:3:7) alisema wanaume wanatakiwa kukaa na wake zao kwa akili sana ili maombi yao yasizuiliwe. Unapoishi na mke wako lazima utumie akili ya ziada, kwasababu mwanamke ni kama mtoto kwahiyo unatakiwa kuwa mvumilivu na kuishi naye kwa umakini. Kuna kipindi mwanamke anaweza akafanya jambo dogo na likakuudhi lakini unatakiwa kumchukulia kama alivyo kwa sababu mwanamke anahitaji uvumilivu, anahitaji kubembelezwa kama mtoto, anahitaji kudekezwa,a anahitaji kupendwa,. Mwanamke kuna kitu anaweza kufanya na ukaona ni cha kitoto na ukakichukuliwa serious, hapo utasababisha, ugomvi ndani ya nyumba.

Unahitaji kumshauri mke wako na kufikia muafaka ili muuishi vyema. Wazazi wetu walitupenda na wakavumiliana na ndio maana leo huu tuna maisha yetu. Jamani hakuna mama hapa duniani, mama ni kama Mungu wa pili hapa duniani. Mama amehangaika na wewe kuanzia alipobeba mimba mpaka sasa una maisha yako. Haha kama mama anafanya kosa lakini bado ni mama yako, unatakiwa kumpenda kwasababu yeye alikupenda na mapak leo unamaisha yako.

Kwahiyo akili lazima itumike katika familia zetu ndivyo tutajenga nyumba zetu vizuri, ndivyo tutakapokuwa na familia nzurii. Hatutakiwa kuwachokoza watoto zetu kwa kuwawekea masharti magumu, watoto wanashindwa kufanya yale wanayoyapenda kulingana na umri wao. Tuonyeshe upendo kwa hawa watoto kwani kesho ndio watakaokusaidia ukishazeeka au kupata ulemavu wowote. Hebu fikiria mama yako angekuwa hakupendi, Je, leo hii ungemchulkuliaje? 

Mungu akusaidie uwe mtu wa kuwakumbuka wazazi wako na hususani mama yako aliyekutunza tangi tumboni mapaka ulipoanza kupata fahamu ya kuwa upo duniani.