RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

15.05.2016: NGUVU HATA NGUVU-SOMO KUTOKA KWA REV. DR. JUSTINE KUTOKA MAREKANI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

SI KWAAJILI YA MAJINA YETU BALI KUJISHUSHA NA KUMUINUA MUNGU AONEKANE
Siku ya Jumapili 15.05.2016 katika ibada ya KUFUNGULIWA Mlima wa Moto Mikocheni, Rev. Doctor Justine Byakweli kutoka Marekani aliweza kuhubiri na hivi ndivyo alivyohubiri, 
“Hatukuja hapa kwa ajili ya majina yetu wala hatukuja hapa kwa ajili ya utukufu wa majina yetu, tumeingia kwa ajili ya Jina la Yesu, na ni yeye tu ndiye tunahitaji aonekane na sisi tushuke. 
Tunahitaji sisi twende chini na Yesu aonekane. Tuombe, Mwenyezi MUNGU Baba yetu siku zote ninakushukuru ulinifanya mtumishi wako, asante kwa kujitoa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu, asante kwa kunipa neema hii ya kusimama hapa na kuyashuhudia makuu yako, mimi ni nani nisimame hapa kukuwakilisha wewe, ni kwasabau ya rehema yako tu, mimi ni mtumishi wako na kanisa ni lako na na hili ni neno lako, mapenzi yako yafanyike katika siku ya leo katika Jina la Yesu Amen.
Rev. Dr. Justine kutoka Marekani

Bwana asifiwe, ninazo shukurani kubwa kwa Mama Askofu Dkt. Gertrude Rwakatare na kwa Mchungaii Machichi nasema asante kwa moyo huu wa upendo na moyo wa Injili ya kazi ya MUNGU, na tangia nimefika hapa nimeuona mkono wa MUNGU, mama asante sana kwa kuliongoza kanisa hili kiroho, watu hawa hawataki wahubiriwe kuhusu Tsunami, wanahitaji waambiwe watabarikiwa, watapata magari, watapata manyumba, lakini hapa tunakuja kutangaza ufalme wa MUNGU, mbingu ipo tunaelekea mbinguni.


ZABURI 84;5-7 Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, na njiia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. Wakipita kati ya bonde la vilio, huliifanya kuwa chem chemi, naam mvua ya vuli hulivika Baraka. Huendelea toka nguvu hata nguvu, huonekana Sayuni mbele za MUNGU.

Hapa dunianii sote tuko katika safari ya kwenda kwa MUNGU, sote tu wasafiri, sote hapa tu wasafiri na sote hapa tu wageni katika dunia hii. Wewe ambaye mawazo yako ymeridhika na nchi yako lakini ujue kuwa hii siyo nchi yako. Nia ya MUNGU ni mimi na wewe twende mbinguni, leo niko hapa kanisani kwa ajili ya kukuonyesha kwamba mimi ni msafiri. Askofu Dr. Gertrude Rwakatare amejitwisha mzigo ili awaoneshhe watu njia ya kwenda Mbinguni. Na ndiyo maana umeacha pombe na mambo ya giza (shetani) ili tuingie mbinguni. 

Mtu anaposafiri ni lazima awe anajua anaenda wapi, na sisi destination au mwisho wetu ni kwenda mbinguni, na kama utaenda mbinguni basi isiwe kuingia tu bali kuishi na Mungu milele. Askofu Dk. Gertrude Rwakatare alipofungua hili kanisa alikusudia kuwaanda watu kuingia Mbinguni. 

Hapa kuna kazi moja tuliyoitiiwa ambayo ni kufufua mioyo iliyokufa ili wote tuwe tunaelekea kwa Yesu, tunaenda mbinguni. Wanaotaka kuelekea mbinguni ni lazima wakiri kwa kinywa chao kwamba Yesu ndiye BWANA na Mwokozi wa maisha yao, uzuri wako hautakufikisha mbinguni, sadaka zako hazitakufiikisha mbnguni, matendo yako mazuri hayatakufikisha mbinguni, kitu kimoja ndio kitakachokufikisha mbinguni ukikiri kwamba Yesu mimi ni mwenye dhambi, na ukikiri Yesu ni Bwana utaokoka na baada ya hapo anza kufuata kannuni na taratibu za Mungu kwa kupitia Biblia yake na mafundisho kutoka kwa watumishi wake aliowaweka hapa duniani.

Tusome ZABURI 84;5 Heri wakaao nyumbani mwako na ambaye nguvu zake zatoka Kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. Kama ulitenda dhambi ama umekimbia hukumu basi ni lazima upitie katika bonde la “hata” ili uingie mahali ambapo utapata uponyaji. Lakini ujumbe wetu unasema “Nguvu Hata Nguvu”, wakati mtu anasema Yesu ni Bwana wa maisha yake ndipo MUNGU anamtia Nguvu. Unapoingia katika utumishi wa MUNGU ndipo MUNGU anakutia Nguvu, lakini hizo nguvu hauzipati kwenye wakati majaribu yanapotokea. 
Mwanadamu anaweza kujaribiwa katika Nguvu, lakini leo ni lazima upitie katika “hata”, hiyo “hata” ni nafasi ya mafundisho, “hata” ni nafasi ya kilio, “hata” ni nafasi ya malalamiko, “hata” ni nafasi ya mabadiliko. Wakati wa uwepo wa MUNGU watu wa MUNGU tunasimama na nguvu zote, tunapotenda dhambi nguvu za MUNGU zinatutoka. 
Unaweza ukawa haukutenda dhambi lakini majaribu hayakufikii, ujue uko katika nguvu na unapitia katika bonde la kilio watu wanadhani unakwisha lakini hautakwisha. Samsoni walimtoa macho wakadhani Samsoni amekwisha lakini hawakujua kwamba siri ya nguvu zake ziko katika kichwa chake, walidhani amekwisha kumbe Samsoni alikuwa bado yuko katika nguvu akapitia katika hata, mara nguvu za MUNGU zikamtoka, lakini alipotubu dhambi akaingia katika jangwa wakamtoboa macho, wakamnyoa, kisha akawaambia mnikamatishe katika nguzo mbili na walisahau kwamba kuna “Nguvu Hata Nguvu”. 
Alipokuwa katika “hata” walimchezea, walimnyoa walimchezea vyovyote vile, ni sawa sawa na mtu akiwa katika “hata” mambo huwa hayaendeki na watu watakucheka, unaweza ukawa katika magonjwa ni “hata”, unaeza ukawa nimfanyabiashara ulikuwa juu na watu wanakusifu mara mali zinaisha uko katika “hata”, katika bonde la kilio, bonde la majuto na machozi, ili umpata MUNGU ni lazima upite katika “hata”. Abrahamu alikuwa hana mtoto lakini akamuomba MUNGU naye akapata mtoto, Abrahamu alipojitoa tu katika machozi ndipo MUNGU kamwambia mimi nataka unitolee Yule mtoto wako ili iwe kwangu sadaka ya kuteketezwa, Abrahamu akaingia katika “hata” kwa kuwa na uchungu.