RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHRISTINA SHUSHO NDIO NAMBA MOJA TANZANIA KWA KUTAZAMWA ZAIDI MTANDAONI


Christina Shusho
Yawezekana licha ya kuwa msikilizaji wa nyimbo na waimbaji mbalimbali wa injili nchini bila kujua kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii namna nyimbo za waimbaji wetu wa Tanzania zinavyofanyika baraka miongoni mwa Watanzania na raia wa kigeni katika nchi mbalimbali.

Hapana shaka ukitaja waimbaji wa muziki wa injili Tanzania wanaofanya vizuri kwa upande wa akina mama, hutakosa kutaja majina kama Bahati Bukuku, Upendo Jbride zamani akifahamika kama Upendo Kilahiro, Rose Muhando, Upendo Nkone, Martha Mwaipaja bila kumsahau Christina Shusho.

Sasa, kwa uchunguzi wa awali uliofanywa na GK umegundua kwamba mwanamama Christina Shusho ndiye anaongoza kwa nyimbo zake kutazamwa zaidi ya milioni 1 kwenye mtandao wa YouTube akifuatiwa na waimbaji wenzake kama Rose Muhando, Bahati Bukuku na Upendo Nkone.
Aidha watazamaji waliowengi wa nyimbo hizo katika mtandao huo wametoa maoni mbalimbali namna nyimbo hizo zinavyofanyika baraka katika maisha yao.

Nyimbo za Shusho ambazo zimetazamwa zaidi ni pamoja na Nipe Macho ( 1,275,172) Umenifanya Ning'are (1, 538,088), Wakuabudiwa (2,122,455). Ambapo nyimbo zote zimewekwa na watu tofauti katika mtandao huo






Chini ni nyimbo za Rose zilizovuka 1 million views





Chini ni limbo wake Bahati uliotazamwa zaidi ya 1 million