RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWANAMUZIKI WA GOSPEL NCHINI KENYA AELEZA KISA CHA KUUBADILISHA WIMBO WA DIAMOND UTANIPENDA NA KUWA GOSPEL SONG




M4J ni mwanamuziki wa injili nchini Kenya na kiongozi wa kundi la Borne Breakers linalowajumuisha wana muziki kama Bahati,Deno,Mr seed na wengine.M4J ameingia kwenye maneno na tetesi nyingi juu hya kitendo chake cha kuamua kuibadilisha nyimbo ya Diamond Platnum iitwayo UTANIPEDA na kuiweka kuwa Gopel song na kuiita UTABADILIKAGA.

Kitendo hiki kilizua maneno mengi na kuchochea ile dhana kuwa muziki wa injili nchini Kenya umepoteza muelekeo kwa kuweka a thin line betweeen Gospel songs na Secular.Ikumbukwe kuwa hivi karibuni mwanamuziki mwingine wa Gospel nchini humo Jimmy Gait aliungana na wanamuziki wengi duniani wakiwemo Joe Thomas(USA),Beka na pipi hawa kutoka tanzania kufanya Cover ya nyimbo ya mwanamuziki wa secular wa nchini MAREKANI aitwaye Adelle, kitendo kilipokelewa tofauti na wapenzi wa Goepel Music nchini humo.
M4J

Tukirudi kwa M4J ambaye kwa sasa ana-roll na nyimbo yake ya MAMBO SAFI, hivi karibuni ameweka wazi sababu za yeye kuamua kuibadilisha nyimbo hiyo na kuwa Gospel, na hapa M4J anafunguka.

“Kwanza kabisa mimi ni mpenzi mkubwa wa nyimbo za Diamond Platnum na alipotoa nyimbo ya UTANIPENDA kwangu mimi ilikuwa ndio nyimbo yake bora kabisa kati ya nyimbo zake zote hususani kwenye upande wa Ujumbe.Hiyo ndio sababu ya mimi kuufanyia cover wimbo huo, nilimuomba Ruhusa Diamond naye akasema its fine.M4J akaendelea kusema UTABADILIKAGA ni Pure Gospel Song ila tu beat na mtiririko wa nyimbo ni Ule ule lakini kwa habari ya ujumbe UTABADILIKAGA ni pure Gospel Song”

Chorous

Je Utabadilikaga

Mungu Akikuinuaga