RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HABARI KUTOKA HASANNA KWANZA: MWIMBAJI WA GOSPEL ALIYESHINDA MILIONI HAMSINI ALISHUKURU KUNDI LA GWT



Melisa Elina John ni Mwanadada mwenye kipaji cha hali ya juu katika uimbaji,amewahi kuwa mmoja wa member wa Kundi la Glorious Worship Team(GWT) linaloongozwa na Emmanuel Mabisa, Melisa alijiunga GWT mara baada ya album ya pili ya kundi hilo iliyoitwa Umenifanya Ibada.Hivi karibuni Melisa ameibuka kidedea katika shindano kubwa la kusaka vipaji nchini linaloratibiwa na Airtel lijulikanalo kama Airtel Trace Music Competition na kufanikiwa kuondoka na kitita cha Shilingi 50,000,000/= (TZS Milioni Hamsini).

Akiongea na Hosanna Kwanza Melisa ambaye anasali katika kanisa la Shaloom Tarbenacle International la jijini Dar es salaam pia anahudumu kwenye Praise Team ya kanisa hilo alisema yafuatayo kupitia maswali na majibu.

Hosanna Kwanza:Melissa kwanza naomba utupe Historia yako kwa ufupi

Melisa John: Mimi Naitwa Melissa Elina John ni Mtoto wa pekee katika familia yetu, nilizaliwa January 29 mwaka 1994 na nimekuwa katika familia inayopenda muziki, na Babu yangu mzaa mama alikuwa Dj Zamani.Nimelelewa sana na bibi mzaa Mama ambaye amenikuza katika misingi ya kumjua Mungu, Kielimu nilisoma Shule ya Msingi pale Mount Kibo kisha O-Level pamoja na A-Level zote nilisoma hapa hapa Dar es salaam katika shule ya Sekondari Loyola(Loyol High School)

Baada ya Kumaliza form six nilisafiri kuelekea nchini Marekani kujaribu Usaili(audition) katika chuo cha Muziki kitwacho Berklee kilichoko Boston. Baada ya Audition nilipita na kutokana na matatizo ya kifamilia nilishindwa kuendelea kukaa kule hivyo nililazimika kurudi nchini.Baada ya kufika nchini niliamua kufanya application za vyuo ndipo nikafanikiwa kupata nafasi katika chuo cha TIA ambapo nipo mpaka sasa nafanya Degree ya uhasibu(Accountancy).


Melissa John

Hosanna Kwanza:Ilikuaje ukaingia kwenye Shindano la Airtel Trace Music Competition 2016?

Melissa John:Ilikuwa ni mara baada ya kuona Tangazo la Airtel Trace music competition kwenye Instagram kisha nikafuatilia kwenye website yao namna ya kujiunga baada ya hapo nikaenda kununua line ya Airtel na kupiga namba yao na nikaimba kama ilivyohitajika nifanye ili kujiunga katika shindano hilo.

Hosanna Kwanza:Ilichukua Muda gani kukujibu kuwa umepita?

Melissa John:Siku hiyo hiyo niliyojirekodi nilijibiwa kuwa nimepita.

Hosanna Kwanza:Unalizungumziaje Shindano la Airtel Trace Music kwa kuwa mashindano Mengine tumeona washiriki wakienda kambini hili likoje?

Melissa John:Hatukuwa na kambi sisi tulikuwa na week mbili za training kwenda kwa mwalimu wa Sauti JOETT na kurudi nyumbani baada ya hapo ilifuata siku moja ya Show ambayo ndio ilikuwa Final namshukuru Mungu sana kwa hilo kwa kuwa Kambi zingekwamisha ratiba zangu Ha haaaaaa (akaachia tabasamu kuhani huyu).

Hosanna Kwanza:Ni kweli ulishiriki BSS?

Melissa John: Yesss nilishiriki BSS mwaka 2013 na nikaibuka mshindi wa tatu.

Hosanna Kwanza:Nini tofauti ya BSS na Airtel Trace Music Competition?

Melissa John:Tofauti zipo nyingi ila tofauti kubwa ni kuw Airtel Trace music inafungua nafasi ya kwenda mbali zaidi na sio kuishia hapa hapa Tanzania.

Hosanna Kwanza:Ni muimbaji gani unayempenda sana hapa Nchini na Nje?

Melisa John: Kwa hapa nchini napenda kazi za Christina Shusho, Angel Benard, Danny Kibambe na Upendo Kilahiro, kwa upande wa Secular Vanesa Mdee yuko vizuri


Melissa John

Hosanna Kwanza:Nini Kinafata baada ya ushindi wako?

Melissa John:Baada ya hapa mashindano yanaendelea huko nchini Nigeria mabako tutakutana washindi kutoka nchi tisa za barani afrika na mshindi atapata nafasi ya kwenda nchini Marekanai na kurekodi na msanii mkubwa Keri Hilson.

Hosanna Kwanza:Nini Matarajio yako ukienda Nigeria?

Melissa John: Aisee natarajia kushinda na kuipeperusha vyema bendera ya nchi yangu.

Hosanna Kwanza:Bado uko katika kundi la GWT?

Melissa John: Hapana kwa sasa sipo tena katika kundi lolote, ninapenda kuishukuru GWT kwa kuwa nimejifunza mengi toka kwao na nimepata marafiki wengi wazuri.Kma ambavyo kifaranga akikua anatafuta chakula chake Melissa nae ameanza kusaka njia yake kama Solo artist na kwa hili nimepata Baraka zote toka kwa Mungu na uongozi mzima wa GWT pia.Shindano la AIRTEL TRACE MUSIC lilianza rasmi mwaka jana 2015 ambapo Andrew Mayunga aliibuka mshindi na amefanikiwa kufanya Colabo na Akon toka nchini Nigeria.

Hosanna Kwanza inamtakia Melisa mafanikiao ya KIMUNGU katika safari yake hii nzima.

Na: Adolph Robert Nzwalla wa Hosanna Kwanza