RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

IBADA YA KISWAHILI LONDON YAWAAGA WATUMISHI WA UBALOZI NCHINI HUMO


Mke wa balozi Kallaghe akiwa na wachungaji baada ya ibada


Katika ibada ya mwanzo wa mwezi inayofanyika kila mwezi katika kanisa la Kiswahili la St Anne's Lutheran jijini London nchini Uingereza chini ya mchungaji Moses Shonga, wiki iliyoisha katika ibada hiyo kulifanyika tendo la kuwaaga waliokuwa watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini humo ambao kwasasa wanarejea nchini kwa kazi nyinginezo watakazopangiwa na serikali.

Watumishi waliofika kuagwa ni pamoja na mke wa aliyekuwa balozi ambaye kwasasa amerejea nyumbani Peter Kallaghe pamoja na familia ya afisa ubalozi bwana na bibi Kiondo ambao wamefanya kazi kwa ukaribu na watanzania nchini Uingereza pamoja na kanisa hilo hasa pale walipochukua jukumu la kuwahudumia waimbaji wa kundi la Upendo Group la Kijitonyama waliptembelea nchini Uingereza miaka ya nyuma.

Aidha kama ilivyoada ya ibada za kila mwanzo wa mwezi hufanyika maombi kwa watu wanaoadhimisha siku zao za kuzaliwa ambapo safari hii ilikuwa kwa waliozaliwa mwezi April na mwezi May ambao walifanyiwa maombi ya baraka. Ibada nyingine inatarajiwa kufanyika tarehe 15 mwezi huu ambao huwa maalumu kwa watu wanaofanya ibada za shukrani ya pekee. Ibada hufanyika kila Jumapili ya kwanza na ya tatu katika mwezi ikishirikisha madhehebu yote na waumini wote hususani kutoka nchi za Afrika mashariki waliopo nchini Uingereza.
Muda: 2.00-4.00pm Mahali: Lovat Lane EC3R 8EE, London.
Mama Kallaghe na Kiondo wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakina mama wa kanisani hap


Mama Nsemwa akizungumza jambo kwa mama balozi Kallaghe

Afisa Kiondo akiwa na mkewe wakisikiliza neno la kuagwa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa baraza

Waliokuwa wakisherehekea siku yao ya kuzaliwa kwa mwezi April na May wakiwa mbele ya keki yao waliyoandaliwa

Picha baada ya ibada, kutoka baraza la vijana la kanisa
Watu walikuwa na furaha ya kupiga picha jumapili