MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MAMBO 19 KILA MWANAUME ANAYATAKA KUTOKA KWA MWENZA WAKE

Haya mambo 19 kila mwanaume anayataka kutoka kwa mwenza wake

USA, New Jersey, Jersey City, Young couple sitting on couch

1. Upendo
Kila mwanaume anataka kujisikia anapendwa. Anataka kuona kuwa mwenza wake anampenda kiuhalisia na anamjali.
2. Heshima
Hata pale anapokuwa hayupo, anataka mwenzake wake awe nyuma yake, kumuongelea na kumheshimu.
3. Uaminifu (Loyalty)
Kila mwanaume anataka mwenza wake awe mwaminifu kwake.
4. Mahaba
Kila mwanaume anahitaji mahaba, na hapa nasema mahaba badala ya ngono, kwasababu si kila mwanaume ni mzuri katika hilo. Mahaba haya yanaweza kuwa kupapaswa, kubusiwa au kukumbatiwa.
5. Kukubalika
Kila mwanaume anataka kujisikia mwenza wake anamkubali kwa mambo mbalimbali kama vile penzi lake, muda, jitihada, anavyojituma na kila anachokifanya kwa mwenza wake.
6. Yeye ni bora zaidi
Anataka mwenza wake kujisikia kuwa yeye ni bora zaidi. Kila mwanaume anataka ajisikie kuwa yeye ni mwanaume bora zaidi kuliko wote aliowahi kuwa nao, na wengine wanataka kujisikia kuwa ni mwanaume pekee ambaye umewahi kuwa naye hata kama anajua si kweli.
7. Uaminifu (Honesty)
Mwanaume anahitaji mwenza wake awe mwaminifu. Uaminifu ni kila kitu kwa mwanaume na kadri mwenzake wake anavyokuwa mwaminifu, ndivyo hawezi kuwa na wivu.
8. Ukweli
Kila mwanaume anahitaji kujua kuwa anaweza kumwamini mwenzake wake na kwamba naye anamwamini.
9. Kulelewa
Sio kila mwanaume anataka mtu atakayempa matunzo kama anayoweza kupata kwa mama yake. Lakini ni kwamba mwanaume anataka kujisikia anapendwa anatunzwa kwa kiwango fulani na mwenza wake.
10. Utulivu
Mwanaume anajua kuwa kuna kiasi fulani cha drama hakiepukiki kutokea wakati wa uhusiano au pale anapooa. Lakini mwenzake wake anapokuwa mtulivu zaidi ndivyo anavyopenda.
11. Anayejitegemea
Hata kama mwanaume anapenda kupata attention kubwa kutoka kwa mpenzi wake, hataki kumuona akiwa kupe, mhitaji sana, au asiyeweza kuwa mwenyewe.
12. Akili
Anataka mwenzake wake aweze kuendelea na mazungumzo na kuwa huru katika mazingira mengi yakiwemo ya kijamii, familia na akiwa naye.
13. Kujiamini
Kila mwanaume hupenda kumuona mwenza wake anajiamini. Hii inamaanisha kuwa anataka mwenza wake ajikubali. Na hapa kujiamini hakumaanishi awe na kiburi.
14. Awe na Mvuto
Kila mwanaume anataka mwenza wake avutie. Mwenzake sio lazima awe kama supermodel bali anayeweza kuyavutia macho yake kila siku.

15. Aive naye
Kila mwanaume anataka kuiva na mwenzake wake na kuhisi kuwa anamvutia. Haoni umuhimu wa kuwa na mwanamke mrembo zaidi duniani bali yule anayeweza kuiva naye vizuri.
16. Mtu wa familia
Mwanaume anataka kujisikia kuwa mwenzake wake anaheshimu kutumia muda fulani na familia yake na kwamba anathamini na kuheshimu pia familia yake. Baadhi ya wanaume huchukulia kigezo hiki si tu muhimu, bali cha lazima katika kumtafuta mwenza.
17. Msimamo
Kila mwanaume anataka mwenza mwenye msimamo na asiyebadilisha mawazo yake kila siku kuhusu kuwa naye na kumpenda. Anataka mwenzake wake awe sawa kihisia na kisaikolojia pia.
18. Ushirikiano
Mwanaume anataka kuona kuwa si yeye pekee ndiye anayefanya kila kitu kuupalilia uhusiano wao. Anataka kuona kuwa kuna usawa fulani kwenye uhusiano.

19. Kujivunia
Kila mwanaume anataka kuona kuwa mwenzake anajivunia kuwa naye. Anataka kumfanya mwenza wake ajivunia na wakati mwingine anahitaji kusikia.
By Anne Cohen – huffingtonpost.com