RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI WA KIROHO WA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE MCH. DK. NIKU KUTOKA ASHEREKEA MIAKA 50 YA HUDUMA YAKE YA UCHUNGAJI SIKU YA JUMAPILI 22.05.2016

MCH. NIKU ASHEREKEA MIAKA 50 YA HUDUMA YAKE YA UCHUNGAJI
Siku ya Jumapili 22.05.2016 Mch. Dk. Niku kutoka Marekani alikuwa anatimiza miaka yake 50 ya hduma ya uchungaji. Sherehe hii ilifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini dar es Salaam Tanzania kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Mch. Dk. Niku ambaye ni Mchungaji wa Kiroho wa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kusimulia historia yake kuanzia shule ya msingi, safari zake za huduma ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kama Zambia, Sweden na Marekani na sehemu zingine Mbalimbali duniani. Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” lilimuandalia keki na ua moja zuri sana, nay eye aliweza kuwalisha wachungaji wa Mlima wa Moto Mikocheni “B” ikiwa ni ishara ya kuwaambukiza upako wa Kihuduma. 
Mch. Dk. Niku

Naye Mchungaji aliweza kumzawadia Bishop Dr. Gertrude Rwakatare zawadi ya kitabu chake cha Jubilee ya miaka 50. Sasa naomba usome ujumbe huu aliokuwa akiongea siku hiyo, alisema, “Bwana Yesu apewe sifa..!!..Nakushukuru sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare  kwani umenipa surprise kubwa mno uliyonifanyia ya kuniandalia keki. Mimi nilipokuwa ninawalisha keki nikaona kweli kwa Yesu kuna utamu. Kuna kwaya moja ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” imeimba na kusema “Kumbukeni ulikotoka”  na mimi ninakumbuka nilikotoka. 
Bahati Bukuku akaimba kuwa “Mimi nimewazidi wote” na mimi ninasema “Nimewazidi wote” kwa miaka na kwa huduma, lakini na nyie wote mmetuzid sisi. Hii ni “Personal statement”. Ni lazima ujijue wewe ni nani na utambue kuwa wewe “Umewazidi wote”, uwe unakaa Kigamboni, Temeke, Mbagala, wewe umewazidi wote. Ngoja nikuambie, Mungu amenibadilishe niseme ushuhuda. Kuanzia, Primary School, kuja mikoche, kwenda Kenya na Marekani. 
Shule za zamani ilikuwa unaingia darasa la kwanza mpka la nane ndipo unaingia shule za sekondari, kila mahali niliposoma shule na nilipokwenda nilikuwa nampenda Yesu Kristo, nah ii nilipenda sio kwasababu ya dini bali Yesu alikuwa rafiki yangu. Nilimpenda Yesu Kristo kwakuwa alinipenda nikiwa na miaka 6, na nilijijua kuwa mimi ni mtoto wa Mungu . 
Leo nikiwa kwenye gari nilikuwa nasema, “Ukiwa mtoto wa Rais unafikiri utahangaika?”, huwezi kuhangaika kwasababu wewe ni mtoto wa mtu mkubwa. Lakini na mimi ni mtoto wa mtu mkubwa aliyeumba mbingu nan chi, na wewe ni mtoto mkubwa aliyeumba mbingu na nchi .

Nilipokuwa naenda Nairobi, watu wakanambia unaenda Nairobi kwenye wahuni..!!!. Leo hii nashuhudia kuhusu huyu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, alikuwa mwembamba na usimuone leo hii yuko hivi kanenepa. Alikuwa ananambia wewe Mch. Niku mshamba, na siku zingine wananiita mke wa Yesu, au mama Superior. Na hawa walikuwa watatu, lakini leo Mungu amewababdilisha wanahubiri Injili. Ninachotaka kukutia moyo ni kwamba usijidharau wewe mwenyewe, hata kama mtu akikudharau lakini wewe usimdharau.

Mimi katika miaka ya 70 wakati wengine mlikuwa bado hamjazaliwa. Niliweza kutafuka kanisa la kuabudia nikapata kanisa la Baptist Church, na nilipofika hapo nikaanzisha kitu kinaitwa “Each One Rich One” ili kushuhudia watu ili niwa-inspire. Mimi maisha yangu ninayoishi ni kwaajili ya kuwa-isnspire watu ili watimize yale Mungu aliyoweka ndani mwao . Ninachojua ni kwamba kila mtu anahazina kubwa mno ndani ya moyo wake au mwili wake, kwani Mungu hajaumba mtu yeyote Yule ambaye ni “Failure” .

Kipindi hicho nilikuwa “Bold” na ile nguvu ya Mungu . Tumesikia leo katika ibada hii dada Safi Nyaule aliyekuwa mchawi akisema yeye alikuwa na nguvu za kichawi zilizomsaidia kutimiza mambo yake.” Na mimi ninasema Mungu akubariki.

Kwahiyo katika ile  “Each OneRich One” nilikuwa nawashuhudia watu kumpenda Mungu. Wakati East Africa Railway wakati inataka kufungwa au kugawanywa, dada yangu akanambia nakuomba uangalie sasa ni kitu gani Mungu anataka kukifanya juu yah ii Railway. Dada yangu alikuwa ni mtu wa imani na ananipenda sana hata ndugu zangu mpaka sasa wananipenda sana na kuniheshimu sana. Dada yangu hata nikiwa nahubiri alikuwa anachukua nguo yangu na kwenda kuwawekea wagonjwa ili wapone, na Mungu kwa kupitia nguo zangu wengi walipona.
 
Kulikuwa na mtu wa West Africa alikuwa akitangaza kuwa kuna kazi zinapatika, nilisafiri kutoka Nairobi kuja Tanzania kupata “Interview” iliyokuwa inafanyika Africana Hotel, wakati tunakwenda kwenye interview na tulipofika huyo baba akasema kwani tutamlipaje?, nikasema mimi mtoto wa Mwakasege kwqsababu natafuta kazi nilimpe tena, nikasema “No Sense”, nikiwa nimekasilika nikasema, “My God has Created nchi yote” na huyu baba anafikiri yeye ndiye anaye-control? Katika interview yetu kulikuwa na wazungu watatu, mmoja alikuwa USAID akaniuliza “You speak English” nakamwambia “Yes” akasema tutakupa kazi USAID, nikashukuru sana. 
Nikaenda Nairobi nikafunga mizigo, nikarudi sikwenda USAID nikaingia ubalozi wa Marekani. Kipindi hicho nikawa sifahamu USAID ni ipi? Mimi nikawa naomba Mungu kuniongoza ila ninachojua ni Mungu tu. Nikaenda “USA Embassy” ambayo zamani ilikuwa ni “Nationa Bank” kwenye ghorofa ya nne. 
Siku moja nikakutana na wale waliotaka kunipa kazi USAID pale “USA Embassy” wakaniuliza, wewe sio ndio tulitaka kukupa kazi USAID? Nikawaambia mimi nilikuwa sijui nikajua wote ni wamoja. Wakanaambia wewe kaa hapa. Kuanzia pale nikawa namshuhudia Yesu Kristo nikaanza kwenda Temeke wakati kipindi hicho Ilala haikuwepo. 
Sisi na mchungaji Taitus kutoka ubalozini tukasema tunakwenda kujenga kanisa ambalo leo ni kanisa la Ilala, tulikuwa tunasema pesa yote inayotoka ubalozini inakwenda kujenga kanisa. Nikasema kuanzia sasa nitakuwa nazunguka kila mahali nikimhubiri Yesu Kristo  hata kama watu walianza kutucheka akiwemo mama Rwakatare.
 
Siku moja nikakutana na mama Rwakatare akiwa ameokoka na kujazwa Roho Mtakatifu nikasema maombi hayarudi bure. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuandaa mkutano mkubwa sana pale UHURU jijini Dar es Salaam, tuliona miujiza ya vipofu kuona, kulikuwa na katoto kadogo kana. Kipindi hicho nilikuwa kijana nikihubiri huyu Yesu.

Mimi huko Marekanini ni m-missionary wa kuwatafuta watu wasisahau kwao, kuyahamasisha mataifa yasimsahau Mungu. Mimi nimemaliza hapa hapa Dar es Salaam. Nakumbuka tulikuwa tunahangaika sana tukizunguka kuhubiri Injili watu waokoke.  Kwasasa nimemaliaza hapa Dar es Salaam kuhubiri nab ado naendelea kuzunguka duniani kuhubiri Injili. 
Tuliweza kufika Kimara katika kanisa la Kimara Assemblies of God lililopo jijini Dar es Salaam kushuhudia, niliweza kushuhudia na kuhubiri, lengo langu sio kuwa na kanisa ila kupanda wachungaji waitwe wachungaji. Ukiitwa kuwa Engineer uwe Engineer, kama ni Mwalimu uwe Mwalimu, kama ni mwanasiasa uwe mwanasiasa lakini mwanasiasa wa Yesu. 
Nikiwa hapa hapa Tanzania nikawa najitahidi kuzunguka kuhubiri na kujitoa kwa kila kitu nilichonancho, marta nikasikia sauti ya Mungu kuwa unatakiwa kwenda kuhubiri, nikauliza, “Mbona nahubiri kila mahali kama vile Kenya, Uganda?” Mungu akanambia, “Sasahivi utakwenda Sweden”, tukiwa tumetoka kushuhudia Kibaha na mch. Bundi katika kanisa la Kiluteli, nikiwa kasichana kazuri, nilikuwa napenda kuvaa vizuri hata watu kutoka American Embassy wakitaka kuvaa nguo za Kiafrika walikuwa wanakuja kwangu.


Nakumbuka nilikuwa na nyumba yangu Magomeni mapipa na kipindi hicho kulikuwa hakuna nyumba nyingi ila kulikuwa na nyumba moja nzuri ya kigae, watu walikuwa wanajaa, watu walikuwa wanapenda kuja kwangu, nilikuwa napenda sana kuwaalika kuja nyumbani kwangu, nilikuwa “Hospitable”  Kwa kukaa na Yesu Hizo zote ni kalama za Mungu, na mapenzi ya Mungu.
 
Baadae niliamu kuhama na kwenda Mikocheni Branding Cinema, huko nikawa na vyumba vingi. Nikamshukur9u sana Mungu na hiyo yote ni kwasababu ya kumtumikia Mungu na  kumshukuri kumshukuru Mungu. Mungu alianza kutenda miujiza hapa Tanzania, na hukonkusunguka kote duniani hakukuanzia Marekani bali kulianzia hapa hapa Tanzania. 
Na kulikuwa hakuna watu wa kunisaidia ila alikuwepo Mungu Baba. Kama wewe ni mtoto wa Mungu unatakiwa kumtumikia kwa asilimia 100, usiwe mtu wa kuja Jumapili na ukitoka kanisani hakuna unachofanya kwa kazi ya Mungu.

Mimi “I Walked, I Talked, I think Jesus Christ, nimuinuaje. Watu wampende Yesu. Nikiwa Kibaha nahubiri  wakati nahubiri watoto wa shule waliweka ramani ya Scandinavia. Unajua unapohubiri “sometimes”  Mungu anakupa mambo Bwana akanambia, “Niondoke Tanzania mnamo July 1977 niende Ulaya”. Nikasema, mimi msichana naenda Ulaya kufanya nini? 
Unajua muongo anamfuata mwanaume, na huyo mwanaume ujue hamjui Yesu Kristo. Hakuna aliyeelewa ila babu na ndugu zangu wa “family”. Dada yangu akanambia kama Mungu amekutuma wewe nenda tu, nikasema, “Kwasababu Mungu amesema nitatii” Nikaondoka Tanzania nikiwa sina hata senti kumi ila nikamuomba Mungu akanipa nauli. 
Nikaelekea Nairobi kuwaaga ndugu zangu na rafiki zangu, baada ya hapo niende Itali nikamuaga dada yangu kwasababu katika akili yangu nilijua ninaenda kufa tu. Kuna mwimbaji Bahati Bukuku leo katika ibada hii ameimba amesema, “Mbeba maono hafi”. 
Nakumbuka kwa mara ya kwanza kumuona Bahati Bukuku ni kipindi kile ambacho alitoa albamu yake ya kwanza akiwa amevaa kilemba kikubwa kichwani na akiwa mwembamba sana. Nakumbuka nilitamka maneno kuhusu huduma yake na kusema, “HUYU ataimba na atarudi nyuma. Na leo nimesikia kutoka kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuwa hajarudi nyuma.

Niliwasiliana na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuwa nataka nije Tanzania katika kusherekea miaka yangu 50 ya huduma, niwaambie watu kuwa “INAWEZEKANA” usirude nyuma, usi-compromise inawezekana kwasabau Mungu wetu ni mkubwa, ni shetani gani atakayenishinda kwa kuwa Mungu alisema shetani yuko chini ya miguu yako. 
That is what I was talking na kufikiria na ndio maana nimeweza kusimama kwa kuwa katika mawazo yangu, namuona Mungu ni mkubwa kwangu, sikupata vishawishi. Kulikuwa na watu wengine walinitegea ili wanikabe ili waniharibu, ila kwa kuwa Mungu alikuwa upande wangu akatuma malaika wake wakashindwa kunikaba.
 
Siku moja nilitoka kusali katika ile sala ya usiki Ilala kanisani hapa jijini Dar es Salaam na kesho yake nikawa na safari ya kwenda Uganda kushuhudia nikasema sasa ngoja nikatishe jangwani ili nifike nyumbani kwangu Magomeni. Wakati nimeacha watu wakiendelea na maombi kanisani. Wakati nakatisha jangwani huku naimba na nimejaa Roho Mtakkatifu, wanaume wawili nyuma yangu wakaniuliza wewe nani? 
Mch. Dr. Niku kutoka Marekani akimkabidhi kitabu chake cha miaka 50 ya Jubilee katika huduma yake ya uchungaji.

Nikajiambia hawa ni walewale Malaya, wakaniambia nisimame, na mimi nikagoma kusimama wala kuangalia nyuma, wakati huo huo kimwili naogopa na nywele zimesimama kwaajili ya hofu. Nikaanza kuongea na Mungu na kusema, “Mungu mimi sitasimama kwasababu unajua nimetoka wapi na unajua kesho nasafiri ninakwenda Uganda” Wanaume hao wakanambia, “Unalinga sio?” Mbele yangu kulikuwa na majani marefu na kamto kama maji. Wanaume hao wakanambia ukifika hapo tutakukaba kwasabau hapo kuna  kagiza. 
Nilipofika katika kale kamto kulikuwa hakuna daraja ila kumweka majiwe kwaajili ya kuvukia, nikakanyaga jiwe la kwanza na la pili, ghafla mbele yangu nikaona mtu mwanaume amevaa kanzu nyeupe anakuja, na alipokaribia kwangu na mimi nikageuza safari ya kwenda nyumbani nikawa namfuata huyo mtu na mbele yetu kulikuwa na makaburi. 
Tulipofika kwenye taa Yule mtu akapotea ghafla na hapo kulikuwa na makaburi. Nilichokifikiria akili nilijua ni jinni. Nikaona ni heri nilirudi kwa wale waliokuwa wanataka kunikaba kuliko kwa huyu mwanaume aliyepotea ghafla.  Nikiwa sijielewi vizuri nikaondoka katika eneo hilo na ghaflla nikaona niko nyumbani kwangu bila kujijua.

Nilipoingia nyumbani kwangu nikawa bado na ule woga na fahamu zangu hazijawa sawa, dada yangu akataka kujua nini kilichonitokea, nikamueleza yote, naye akaniambia, “Dada siumeokoka?, Mungu alikutumia malaika wakuokoe. Nikajiambia kuwa Yule hakuwa malaika ila alikuwa Yesu mwenyewe.
 
Ninachotaka kusema ni kwamba, majaribu ni mengi na nimeyapitia mengi, lakini ninamshukuru Mungu kwakuwa amenilinda. Nikaondoka Sweden nikawa bado ninamuomba Mungu anisaidie ninunue magitaa kwaajili wanakwaya, nipate pesa kwaajili ya kusaidia makanisa. Bado ninamuomba Mungu. Katika kitabu change nimeandika MIUJIZA BILA KUONA. 
Nikiwa Sweden nikaenda katika ubalozi wa Tanzania na kuwaambia mimi ni Mtanzania nimekuja kuhubiri Injili, wakanicheka sana, wakashangaa kwasabau wengine wanaenda huko kutafuta kazi halafu mimi nimeenda kuhubiri. Nikawaomba wanisaidie kutafuta kazi ya kujishikiza kwasababu lengo langu lilikuwa kuhubiri Injili na ninaishi kwa IMANI, ila nahitaji kupata pesa ninunue magitaa ya kanisani, wakaniuliza, “Wewe una familia?”, nikawajibu “ndio” . 
Lakini akili yangu ilikuwa kusaidia watu wa Mungu kundelea kumtukuza Mungu. Nikiwa hapo Ubalozini wakanambia kuna kazi lakini wanahitaji mtu anayejua Kiingereza, Kiswidishi na Kifaransa, nikawaambia “Ok sawa”. Nikajiambia moyoni hajilishi wanataka watu hao ila mimi ninachojua ni kazi yangu, na pesa nitakazopata si kwaajili yangu ni kwaajili ya kazi yako Mungu. Baada ya hapo wakanambia “Njoo uje kufanya kazi” Nikaanza kufanya kazi pale Ubalozi, lakini ikawa bado, kwani nilikuwa nahitaji kurudi Tanzania.

Nikiwa nimerudi kutoa Sweden, mimi na wanawake wengine akiwemo Bishop Dr. Gertrude Rwakatare tukafanya mkutano katika ukumbi wa Lumumba Hall hapa jijini Dar es Salaam. Akaja mama Sofia Kawawa, kwahiyo tulikuwa tunasghulika na wakuu wa siasa na ukumbuke tulikuwa bado tunajishughulisha na siasa. Hata kama mimi nilizaliwa kijijini kwenye kajumba na maji kuyapata ni mpaka uende mile nyingi, lakini nilijua ninachokifanya ni kwaajili ya MUNGU.
 
Ninachotaka kukuambia ni kwamaba Mungu anapokubariki mtolee sadaka ya shukrani kwani atakubariki zaidi

Wakati nahubiri katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam nikijianda kwenda Mwanza kuhubiri, kuna vijana wawili wataka niende Zambia kuhubiri nikawaambia haitawezekana kwasababu naenda Mwanza. Wakati naenda kukata tiketi katika kituo cha Railway karibu na headquarter ya Police hapa Dar es Salaam, Mungu akanambia huendi Mwanza unaenda Zambia. Nikajiuliza mbona hawa watu siwafahamu?

JE, UNGEPENDA KUJUA KAMA ALIENDA ZAMBIA NA KILIFANYIKA NINI HUKO
JE, UNGEPENDA KUJUA SAFARI YAKE YA SWEDENI NA MIKASA GANI ILIMKUMBA
JE, INGEPENDA KUJUA SABABU GANI ILIMFANYA ATOKE SWEDEN NA KWENDA MAREKANI?
JE, UNATAKA KUJUA KITU GANI KILIMSABABISHIA YEYE KUTAKA KUJIUA NA NI NANI ALIMUOKOA?
JE, MALENGO YAKE NI YAPI MPAKA SASA KATIKA HUDUMA YAKE?
USHAURI GANI AMEUTOA KWETU SISI?

BASI TEMBELEA: Youtube kwa jina la Mlima wa Moto au Rulea Sanga au tembelea blogu yetu www.mountainoffire .blogspot.com angalia Video au ingia Facebook kwa jina la Mountainoffire Tanzania

MUNGU AKUBARIKI SANA

MATUKIO YA KUPOKEA UA NA KULISHWA KEKI