MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MKUU WA MKOA MH. MAKONDA ANESEMA MUNGU AMEMPA NJIA YA KUWAPATA WATUMISHI HEWA 2019

Mei 2 2016 Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda amewaapisha wakuu wa idara na maofisa utumishi wote wa manispaa hiyo ili kusaidia kubaini watumishi hewa.

Makonda kafikia hatua hiyo baada ya watumishi hao kuwa wanampa idadi tofauti kila anapohitaji kupata taarifa, akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaamMakonda anasema..

‘Mara ya kwanza mliniambia tuna watumishi hewa 71, mara ya pili mkasema 87 na mara ya tatu wakapungua hadi 66 tena mara zote hizi ni idadi ya watumishi hewa kimkoa jambo ambalo roho wa Mungu alinikataza kutangaza‘

‘Sasa Mungu kanipa njia ambayo nimewaambia wiki iliyopita, Leo hii wameongezeka wamefika watumishi hewa 209 huku ziai ya bilioni 2 zikipotea. Je, nisinge msikiliza Mungu si mgenifanya nikafukuzwa kazi?‘

Baada ya maelezo hayo Mkuu wa mkoa akawapatia mikataba ya viapo katika kutafuta watumishi hewa, lengo likiwa ni kuwataka kila mtumishi kuwabainisha watumishi wao hewa katika idara zao na atakayebainika kutoa taarifa zisizo sahihi mkataba umfunge mwenyewe. 
Watumishi wakila viapo mbele ya Mkuu wa mkoa
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda