RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MLIMA KILIMANJARO WATUNUKIWA ZAWADI YA KIVUTIO KIKUU

Mlima Kilimanjaro.

MLIMA Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi barani Afrika, umetangazwa kuwa kivutio kikuu cha utalii katika bara katika mwaka 2016.

Hili lilitangazwa katika hafla ya taasisi ya masuala ya utalii Afrika na eneo la Bahari ya Hindi ijulikanayo kama World Travel Awards Africa and Indian Ocean iliyofanyika Zanzibar wiki iliyopita.
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jana ilisema hafla hiyo ilihudhuriwa na mamia ya viongozi wa masuala la utalii iliyoandaliwa na kampuni ya Diamonds La Gemma Dell’est na kufanyika huko Nungwi, Zanzibar, Jumamosi iliyopita.

“Bodi ya Utalii ya Tanzania, imepokea kwa heshima kutangazwa Mlima Kilimanjaro kuwa ndiyo kivutio kikuu cha utalii barani Afrika. Uteuzi huu ni dhahiri utachangia juhudi zetu za kuendeleza utalii nchini Tanzania, hususani kwa kuufanya ulimwengu ufahamu kwamba Tanzania ndiyo mmiliki wa Mlima Kilimanjaro ambalo ni kivutio kikuu barani Afrika,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Source: Allafrica.com