RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RC PAUL MAKONDA KUHUSU WAMACHINGA WA DAR NA MAENEO YAO MAPYA…(+VIDEO)


Ni siku kadhaa tangu wafanyabiashara wadogo wadogo (Wamachinga) kuondolewa kando kando mwa barabara na kupelekwa kwenye maeneo yao husika yaliyotengwa naSerikali.

Najua nina watu wangu mnataka kufahamu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda atazungumza nini juu ya maeneo hayo husika….’Kwa upande wafanyabiashara ndugu zetu wamachinga hakuna Serikali yenye nia mbaya nao lakini tunachotafuta kuhakikisha mazingira au kutengeneza kila mmoja kufanya kazi katika maeneo yao maalum na sio tu wamachinga bali hata watu wengine’- Paul Makonda

‘Kwahiyo nawaambia kwamba hatuna nia mbaya na kule wanapokwenda tutaendelea kuhakikisha mazingira yao yatakuwa mazuri zaidi na zaidi, lakini ningependa kuwaambia watanzania waache tabia ya kununua vitu bila kuwa na risiti kwani ni muhimu kuwa na risiti ili baadae’ – Paul Makonda