MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

UTEUZI MWINGINE ALIOUFANYA RAIS JOHN MAGUFULI LEO MAY 30 2016Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Serikali ambapo amemteua Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi, uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Uteuzi wa Anne Semamba Makindaambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology – DIT).

Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake, uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.