RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIDEO: BAADA UHUSIANO WA CUBA NA MAREKANI KUREJEA HII NDIO HATUA WALIYOANZA NAYO



Ni zaidi ya miongo mitano Cuba na Marekani hazikuwa katika uhusiano mzuri lakini hivi karibuni Rais wa Marekani Barack Obama alifanya ziara ya siku 3 iliyolenga kurekebisha uhusiano huo, ziara hiyo ilikuwa ni ya kwanza tangu Calvin Coolidge ambaye alitembelea wakati wa vita mwaka 1928.

Baada ya ziara hiyo, leo May 02 2016 imeanza kuonesha matunda ambapo Meli ya kifahari iitwayo Adonia ya Marekani imeanza safari yake kuelekea Cuba ikitokea nchini Marekani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita ikiwa na abiria wapatao mia saba.

Safari hiyo ya meli imeonekana ni hatua kubwa katika kuimarisha uhusiano wa Cuba na Marekani baada ya serikari ya Cuba kukubali kuondoa zuio la raia wake kuingia nchini Marekani ama kutumia maji kama njia ya usafiri kuingia nchini humo