MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

DADA ANAYEISHI NJE YA TANZANIA APONA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI, KUTOKULA CHAKULA, KUTOPATA USINGIZI KWA MUDA WA MIEZI MIWILI BAADA YA KUKANYAGA MLIMA WA MOTO

Siku ya Jumapili 22.05.2016 dada huyu aliweza kushuhudia jinsi Mungu alivyomkomboa katika ibada ya UKOMBOZI Mlima wa Moto Mikocheni “B” baada ya kutamkiwa maneno ya kinabii kutoka kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwamba aonane na wachungaji na wainjilisti wamuombe na hapo atapokea uponyaji, na hivi ndivyo alivyoshuhudia, “Siku moja nilikuja mahali hapa na baba yangu ndiye aliweza kufika katika madhabahu hii ya Mlima wa Moto akiwa ameongozana na mimi, lakini mimi sikuweza kuzungumza lolote . Baba alipomaliza kuongea ikabidi twende kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, na yeye akatuambia tuwe tuna kuja hapa kanisani mara kwa mara na kuwaona Wainjilisti na Wachungaji ili watuombee kila siku. Na sisi tukawa tunakuja na kuombewa na wachungaji hapa kanisani. Tatizo langu nilikuwa siwezi kulala, siwezi kula, na kwa kipindi cha wa miezi miwili hivi nilikuwa siwezi kulala kabisa wala kupata usingizi. Nilikuwa nasikia sauti, kila ninapotembea, nasikia watu wananiita, shetani ananiongelesha ninashindwa kulala wala kula, lakini namshukuru Mungu baada ya maombezi ya Mlima wa Moto sasa naweza kula na kulala. Naomba mzidi kuniombea..Amen
 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare (kulia) akiwa na dada mwenye ushuhuda
 Mch. Noah Lukumay (kulia)