MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

ABDI KASSIM KAITWA TENA MALAYSIA KUFANYA MAJARIBIOKama wewe ni mpenda soka najua jina la Abdi Kassim Sadallah maarufu kama Babi auBallack wa Unguja sio jina geni masikioni mwako, kama hujui Abdi Kassim Babi kwa sasa yupo Malaysia anafanya majaribio katika klabu ya ATM ya Ligi Kuu Malaysia, millardayo.com ilifanya exclusive interview na Abdi Kassim kutokea Malaysia.

“Ni kweli nimerudi Malaysia katika klabu ya ATM hii sio niliyokuwa naichezea mwanzoni, mwanzoni nilikuwa nachezea UiTM, nina wiki mbili za majaribio tayari wamenikubali na mungu akipenda wiki ijayo watanipa mkataba kwa tupo wachezaji kama wanne tunafanya majaribio na tunahitajika watatu, mimi wanaonekana kunikubali”

Timu anayofanya majaribio Abdi Kassim ipo nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu Malaysia.

Abdi Kassim mwishoni mwa mwaka 2015 alikuwa akiichezea klabu ya UiTM, lakini alirudiZanzibar baada ya kumaliza mkataba na klabu hiyo, kama utakuwa unakumbuka vizuriAbdi Kassim ndio mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga goli kwa mara ya kwanza katika uwanja mpya wa Taifa, alifunga mwaka 2007 katika mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Uganda The Cranes.