MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

GOODLUCK GOZBERT AKANUSHA KUMUANDIKIA WIMBO RICH MAVOCAL


Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Goodluck Gozbert amekanusha uvumi unaoenea nchini kuwa yeye ni mmoja kati ya waadishi wa nyimbo ya Imebaki story ya Rich Mavoko.Goodluck amekanusha uvumi huo pindi alipokuwa akifanya mazungumzo na kituo cha redio cha Kings Fm, sambamba na hilo Goodluck amesema yeye sio muandishi wa nyimbo za secular ila pindi akipata melody na wimbo huamua kumpa mtu yeyote kama alivyofanya kwa Ben Paul na wimbo wa Moyo Mashine.

Goodluck ni Producer, mwandishi wa nyimbo na muimbaji wa nyimbo za injili, ama kama anavyojulikana pia kama Lollypop, amekanusha kuandika wimbo wa Rich Mavoko, Ibaki Story.Tetesi hizo zimekuwepo wiki hii mwanamuziki Rich Mavoco na kudai kuwa kuna vitu kadhaa Lollypop aliweka kwenye wimbo huo lakini si kwamba aliandika.Akiongea na kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka, muimbaji huyo alisema:

Mavoko tunafahamiana na tumewahi kuonana mara chache lakini kuhusu hiki kinachoendelea kutrend kwakweli sifahamu na tumewasiliana pia kuhusu hili akaniambia anashangaa, nikamuambia mimi pia nashangaa kuhusu hilo kwahiyo ni kitu ambacho sielewi kimetokana na nini na ni kwanini kinazungumzwa.”

“Ni tetesi tu na hazina ukweli wowote,” amesisitiza.