RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA DEITRICK HUDDON KUANZA IBADA ZA KILA JUMAPILI


Baada ya miezi mitatu kupita toka Mwanamuziki, Actor na mtumishi wa Mungu Deitrick Huddon kutangaza kufungua kanisa na kuanza na ibada za kila alhamis jioni, Deitric ametangaza rasmi kuwa kanisa lake litaanza ibada za kila jumapili.Kupitia ukurasa wake wa Instagram mwanamuziki huyo amaesema ametoa taarifa hiyo na kufungua ukurasa mpya wa maisha yake kama mchungaji wa kanisa lake liitwalo Hill City Church lililoko jijini Los Angeles nchini Marekani.

Kupitia ukurasa huo Detrick ametanabaisha yafuatayo na hapa namnukuu “Join me and the team every Thursday for a night of crazy worship and a prophetic word from the Lord! The wait is over L.A! Ready or not here we come!” Hivi karibuni Deitrick Huddon kwa kutumia Muvie series yake iliyojipatia umaarufu ya PREACHERS OF LA alijikuta matatani mara baada ya watumishi wengi wa Mungu kutopenda alichofanya.



Katika Series hiyo Deitric aliweka wazi maisha ya wachungaji nje ya madhabahu.Imezoeleka kuwaona wachungaji jumapili wakihubiri na kuteka hisia za watu, humo ndani ya series kuna vituko na maisha halisi ya watumishi wa Mungu nje ya Altar.Pamoja na yote kumtumikia Mungu ni jambo jema na yeyote afanyayo hayo ana akili Njema,all the best to Him.