MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MANJI ATIBUA HOTUBA YA MGENI RASMI


Nicodemus Jonas na Wilbert Molandi

JUZI Jumamosi wanachama wa Yanga walifanya kituko kisicho cha kawaida kwa kushindwa kujizuia baada ya kuacha kusikiliza nasaha za mmoja wa wageni rasmi aliyekuwa akitoa neno na kulipuka ghafla kwa kelele kubwa, shangwe na vigelegele baada ya mgombea uenyekiti, Yusuf Manji kuingia ukumbini.

Kituko hicho kilijitokeza kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo, Diamond Jubilee ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Revocatus Kuuli, alipokuwa akitoa neno kwa niaba ya TFF, lakini kitendo cha Manji kuingia ukumbini majira ya saa 6: 13 mchana, ukumbi mzima ulilipuka kwa kelele nyingi, hali iliyomlazimu Kuuli kusitisha kuongea mpaka walipotulia tena, kitendo kilichochukua takribani dakika tano kutekelezeka.

Hakika hiyo ilikuwa ishara ya kukubalika kwa kiongozi huyo aliyepewa ridhaa tena kuendelea kuwa mwenyekiti wao kwani hakuna kura hata moja iliyomkataa kwenye uchaguzi huo.

Mwisho wa matokeo, kelele za kumshangilia kweli zilikuwa na maana kutokana na kura alizorundikiwa ambapo ziliharibika kura mbili tu kati ya kura 1470 zilizopigwa.