RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIDEO: MCH. FRANCIS MACHICHI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI HIVI NDVYO ALIVYOFUNDISHA JUU YA KUSIKIA SAUTI YA MUNGU ILI IKUSAIDIE KATIKA MAAMUZI SAHIHI



Kuna mambo mengi aliweza kuyahubiri katika ibada ya habari njema ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni siku ya Jumapili 12.06.2016. Sasa naomba tumsikilize kwani kuna mambo mazito aliweza kuhubiri

ANGALIA VIDEO HII MUHIMU SANA KWAKO



MAHUBIRI HAYA YANATOKA KATIKA CLIP HAPO JUU

Siku ya Jumapili ya tar. 12.06.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Francis Machichi aliweza kufundisha juu ya " NAMNA YA KUSIKIA NA KUELEWA SAUTI YA MUNGU ILI IKUSAIDIE KUFANYA MAAMUZI SAHIHI " , alisema, 
Tukiangalia mtumishi wa Mungu Daudi alipokuwa akivamiwa na Wafilisti, akamuuliza Mungu, nifanye nini? Na Mungu akwambia, nenda nitawatia mikono mwako. 
Mch. Francis Machichi

Na Wafilisti walipokuja mara ya pili, Mungu akamwambia Daudi , “Nenda ukapigane nao, lakini sasa usiende kwa mbele bali nenda nyuma na Mimi nitawatia mikononi mwako”. Kwahiyo Daudi alisikia sauti ya Mungu na kuielewa na ikamsaidia katika uamuzi wake wa kupigana vita wa Wafilisti na hatimaye akavishinda.
Mzee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Mzee Malya

Kuna njia tatu kubwa ambazo Mungu tumia kufikisha sauti yake kwetu, na jia hizo ni:
1.Neno Lake
2.Ndoto
3.Watumishi wake 
NENO LAKE
Ukisoma 2Timotheo:13:6-17. Biblia inasema kila andiko lilipewa kwa pumzi ya Mungu, linafaa kwa mafundisho, kuongoza n.k . Kwahiyo Mungu anatumia sana Neno lake ili tuweze kusikia sauti yake. Na hii ni njia yake kubwa ambayo Mungu anatumia kufikisha sauti yake kwetu

NDOTO ukisoma Hesabu 12:6. Kisha akawambia sikilizeni maneno yangu aakiwepo Nabii katikakti yenu mimi BWANA nitajifunua kwake kwa njia maono.

Ndoto ni lugha ya picha tena ni rahisi kuielewa ambayo Mungu hutumia kwako ili kufikishia ujumbe wake. Unaweza ukalala lakini kwenye usingizi wako ukaona kuna kitu kinaendelea. Mungu hutumia sana ndoto lakini naye shetani hutumia ndoto. 
Unaweza kusikia sauti ya Mungu kwa kupitia ndoto lakini shetani naye hunyemelea watu kupitia ndoto. Mimi kama mchungaji wako huwa sitaki kusikia sauti ya shetani na ninataka na wewe usisikie kwa jina la Yesu. Mungu hutumia njia nyepesi sana kukuletea ujumbe kwa njia ya ndoto, kwa mfano anakuletea picha fulani au tukio fulani ambalo wewe ni rahisi kulitambua. 
Sasa unapoota hiyo ndoto ujue kuna mambo inabidi uyafanye kutokana na hiyo ndoto. Soma Ayubu 33:14, Kwa kuwa Mungu hunena mara moja na hata mara ya pili ajapo kuwa mtu hajali katika ndoto, katika maono, katika usingizi mzito ukiwa kitandani. Kwahiyo hata mazingira yako ya kulala yanaweza kusababisha kusikia sauti ya Mungu.

“Mungu anaweza kusema na wewe kupitia neno lake na pia kwa njia ya ndoto. Katika ndoto lazima uzingatie mambo mawili, kwanza, ndoto ukiona ni nzuri au inavutia, basi unatakiwa kumwambia Mungu kwamba, 
“Kupitia ndoto hii naomba mipango yangu itimie kwenye maisha yangu”, pili, lakini ukiona ni ndoto ambazo ni mbaya ambazo zinaletwa na adui shetani (kama vile ndoto za kifo, ndoto chafu, ndoto ambazo hazieleweki) basi mwambie BWANA “Ninakataa hizi ndoto zisitimie katika jina la Yesu Kristo”. Hatuwezi kupata maneno mazuri pasipo kuelewa sauti ya Mungu.

WATUMISHI WA MUNGU
Tunasikia sauti ya Mungu kupitia watumishi wake hapa duniani. Na sisi watumishi wa Mungu ukiona tupo hapa kukuhubiria na usituchukulie kirahirahisi kwani kuna kitu tumebeba cha kumpendeza Mungu. 
Unaweza kuniona mtumishi wako sina chochote, sivai kama unavyopenda wewe, siongei unavyopenda wewe, sisemi unavyosema wewe au unavyopenda ni sema kama unavyotaka niseme; l;akini Mungu anatuweka mahali hapa kwasababu anatukubali kwa njia moja au nyingine ili tukufikishie ujumbe. 
Kwahiyo ukitaka kusikia sauti ya Mungu, simama na usikilize kile kinachotoka madhabahuni ambako Mungu anaongea na wewe kupitia wachungaji wake. Usinagalie mchungaji wako nilivyovaa, usikie Kiswahili change kibovu, usinagalie sura yangu ni mbaya, wala usiangalie ufupi wangu, lakini Mungu anasema ukitaka kusikia sauti yake, 
uwasikie watumishi wa Mungu ambao wanasima madhabahuni kwa kibali cha Mungu, na Mungu anawakubali kwa njia moja au nyingine. Ndugu zangu sisi watumishi wa Mungu tunanafasi mbele za Mungu. Mumngu mwenyewe anasema ninawapenda wale wanaompendeza Mungu. Je, wewe unampendeza Mungu?