RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MRS JAN CROUCH MUASISI WA TBN ATANGULIA MBELE ZA HA


Mrs Jan Crouch maarufu kwa jina la Momma Jan mmoja wa waanzilishi wa kituo maarufu cha Television cha Trinity Broadcasting Network (TBN) amefariki jana nchini Marekani.Kwa muhimu wa taarifa zilizotolewa na mwanaye jumanne wiki hii zinasema kifo cha Mooma Jan kimetokana na Stroke na hivyo ataungana na Mumewe Mr Jan Crouch aliyetangulia mbele za haki mwaka jana 2015.
Momma Jan na Mumewe Paul enzi za Uhai wao

Mrs Jan Crouch amefariki akiwa na umri wa mkaka 78,Momma jan kwa Kipindi kirefu amekuwa kipenzi cha wengi na hii ni kwa misingi yake ya ualimu wa Neno la Mungu.TBN kwa sasa inaaminika ndio kituo Bora cha Television duniani na kimefikia nchi nyingi zaidi duniani kote.

Momma Jan na Mumewe Paul kwa pamoja walianzisha TBN mnamo Mwana 1973 toka miaka hiyo mpaka leo TV hiyo imepitia hatua mbalimbali mpaka Kuwa kituo cha Bora cha cha kikristo cha Television duniani.Wawili hawa mtu na mumewe wamefanikiwa kuacha alama duniani kazi imebaki kwako na kwangu, Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina lake libarikiwe.